January 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nahodha Yanga: Tupo tayari

Lamine Moro

Spread the love

LAMINE Moro, Nahodha wa klabu ya Yanga amesema kuwa wako tayari kwa ajili ya kuwakabili klabu ya Simba kwenye mchezo wa kesho ikiwa ni muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa katika Uwanja wa Mkapa, Jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

“Kesho tuna mechi kubwa dhidi ya Simba, tumejiandaa vizuri na tupo tayari kuwakabili wapinzani wetu,” amesema Lamine.

Nahodha huyo amesema hayo leo kwenye mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), katika kuelekea mchezo wa kesho.

Mchezaji huyo ambaye atakuwa anacheza ‘derby’ yake ya tatu toka alipojiunga na Yanga kwenye msimu wa 2019/20 na kupoteza mchezo mmoja akiwa uwanjani.

Lamine ambaye ameonesha mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga toka uliponza msimu huu na ataiongoza safu ya ulinzi ya klabu hiyo kwenye mchezo wa kesho ambapo mpaka sasa wameruhusu mabao 2, kwenye michezo tisa waliocheza.

error: Content is protected !!