January 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nafasi ya Mkapa yapata mrithi UDOM

Marehemu Benjamin Mkapa

Spread the love

BALOZI John Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi nchini Tanzania, amesimikwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Anaripoti Hamisi Mguta…(endelea).

Kabla ya nafasi hiyo kutwaliwa na Balozi Kijazi baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli, mkuu wa UDOM alikuwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa aliyefariki dunia tarehe 24 Julai 2020.

Balozi Kijazi aliuliwa na Rais Magufuli tarehe 21 Agosti 2020 kushika wadhifa huo.

Balozi John Kijazi

Gaudencia Kabaka, Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho amemsimika Balozi Kabaka kwenye mahafali ya 11 yaliyofanyika leo Alhamisi tarehe 17 Desemba 2020 jijini Dodoma.

Baada ya kusimikwa, Balozi Kijazi amesema milango ipo wazi kwa ajili ya kuwasilisha changamoto zinazokikabili chuo hicho huku akisisitiza kufuata taratibu zilizowekwa na chuo hicho.

error: Content is protected !!