Tuesday , 19 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Nabii wa Ngono mbaroni Dodoma
Habari MchanganyikoTangulizi

Nabii wa Ngono mbaroni Dodoma

Spread the love

JESHI la polisi mkoani Dodoma, limemkamata Onesmo Machibya (44), maarufu kwa jina la Nabii Tito, kwa madai ya kinachoitwa, “kueneza chuki ya kidini dhidi ya wengine.”Anaripoti Dany Tibason.

Nabii Tito ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ng’ong’onha, mkoani humo alikamatwa jana na jeshi la polisi baada ya picha zake za video za akitetea zinaa, pombe na starehe nyingine za kidunia, kwa kutumia kitabu kitakatifu cha Bibilia.

Nabii Tito anasema katika video hiyo, kuwa mwanamme wa kikiristo, anaruhusiwa kisheria, kuoa mfanyakazi wake wa ndani (kijakazi); kunywa pombe, kuoa wanawake zaidi ya mmoja na mambo mengine kadhaa ambayo ukirsto umedaiwa kuyakataza.

Aidha, nabii huyo anadaiwa kusambaza vipeperushi vinavyohamisha mambo hayo katika maeneo ya starehe; kutangaza imani ya dini inayokiuka maadili ya nchi na kufanya hadharani vitendo vya “udhalilishaji,” huku akitumia kitabu kitakatifu cha Biblia.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi, mahubiri hayo ya Nabii Tito, ni kosa la jinai kwa kuwa linachochea chuki dhidi ya wakirsto wengine na kinyume cha kifungu cha sheria Na.129 cha kanuni ya adhabu Sura ya 16 ya mwaka 2002.

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amemtuhumu Nabii Tito kutumia vibaya Biblia kwa kutoa tafsiri za upotoshaji, kufanya vitendo vya udhalilishaji hadharani na kuchochea maovu katika jamii.

Amesema Nabii Tito amekuwa akishirikiana na wanawake wawili ambao anawaita wake zake, mmoja wao akidai kuwa kijakazi wake.

Hata hivyo, kamanda Mroto amesema, uchunguzi wa awali uliofanywa na Dk. Dickson Philipo wa hospitali ya wagonjwa wa akili Mirembe aligundua kuwa mtuhumiwa huyo ni mgonjwa wa akili kwa muda mrefu.

Amesema nabii huyo aliwahi kufanyiwa uchunguzi tarehe 6 Juni 2014. katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili na kugundulika ana ugonjwa wa akili.

Amesema akiwa Muhimbili alitibiwa magonjwa ya akili ambapo aliruhusiwa kutoka wodini na daktari wake aliyetambulika kwa jina moja la Dk. William ambapo alitakiwa kurejea tena kwa uangalizi wa tiba tarehe 9 Julai 2014, lakini hakuweza kurejea.

“Baada ya jeshi la Polisi kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa anaonekana Dodoma akifanya vitendo vya kizalilishaji pamoja na kupotosha jamii ndipo tulimkamata na kumpeleka katika Hospitali ya Mirembe kwa uchunguzi zaidi.

“Baada ya uchunguzi uliofanywa na Dk. Dickson Philipo wa hospitali ya Mirembe tumegundua kwamba ni mgonjwa wa akili kwa muda mrefu,” amesema.

Kamanda huyo wa polisi ameshangazwa kuwa pamoja na mtuhumiwa kuwa na hali hiyo, ameendelea kuhamasisha maovu yaliyo kinyume na mema ya dini zote na desturi za Watanzania huku akionekana ni mtu mwenye akili timamu.

“Jambo la kushangaza kuna watu wanamshabikia na kuambatana nae Jeshi la Polisi litawachukulia hatua kali watu hao kwani ni kinyume na tamaduni za Kitanzania,” amesema.

Kamanda Muroto amesema, jeshi lake linaendelea kumshikilia Nabii huyo kwa ajili ya upepelezi zaidi na kunusuru maisha yake.

“Tunamshilia Nabii Tito kwanza kabisa tunanusuru maisha yake kwa kuwa watu wenye dini hii wanaweza wakaona wanadhalilishwa hivyo wanaweza kumdhuru pili anaonekana ni mgonjwa wa akili lakini anaonekana anafanya makosa ya kijina hivyo tunamfanyia upelelezi zaidi,” amesema.

Naye Nabii Tito akizungumza katika ofisi za jeshi la polisi mkoani humo na mbele ya maofisa wa jeshi hilo ameendelea kusisitiza kuwa anachokizungumza, hakitoki kichwani mwake; bali ni maneno yaliyomo kwenye Bibilia.

Amesema, “kanisa langu na waumini wangu lazima wawe na shepu nzuri, ikiwemo kuwa na sura nzuri, kwa sababu watasadiki kile ninachokizungumza. Ninachokizungumza, ndicho kilichomo kwenye Bibilia.”

Nabii Tito amesema kwa sasa yupo mbioni kumtafuta msanii maarufu hapa nchini Wema Sepetu kwa sababu anaimani atashawishi wengi kuingia katika kanisa lake ambalo analiabudu ambalo lipo katika eneo la Ng’ong’ona mkoani Dodoma.

Akizungumzia kuhusiana na mambo anayoyafanya amesema yeye anatumia muda mwingine kuoa wafanyakazi wa ndani ya nyumba, pamoja na kufanya matendo ambayo ni kinyume na maumbile jambo ambalo halimtatizi kabisa.

Amesema yeye anawafanyia watu hivyo, lakini na yeye inabidi afanyiwe ili aweze kusamehewa dhambi ambayo anaifanya kwa sasa.

Hata hivyo amesema kuhusu pombe anazokunywa kwake sio tatizo na waumini wake wakiingia kanisani hupewa pombe ikiwemo kutoa sadaka na ukinywa kama hujalewa anakurudishiwa pesa yako.

Tito ameemdelea kusema sasa yuko katika kampeni za kuhakikisha anaendeleza yale yote anayoyasadiki kwa sababu anaamini sio dhambi kabisa.

Amesema yote anayoyafanya yeye ikiwemo kufanya michezo mibaya kwa watu, basi na yeye anarudishiwa na watu wengine, ili kusafisha dhambi anayotemba kabla hajahukumiwa.

Katibu wa Umoja wa Madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma, (UMKD) Askofu Dk. Eliya Mauza amesema umoja huo hawawezi kukubali udhalilishaji unaofanywa na Nabii huyo na kulitaka Jeshi la Polisi kumchukulia hatua kali zaidi.

“Mungu ni mtakatifu Umoja wa Madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma hili hatuwezi kulikubali hata kidogo na tunaliomba Jeshi la Polisi lizidi kuchukua hatua hali kwa mtu huyo,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the loveSUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu,...

Habari Mchanganyiko

Bunge laja na Marathon kuchangia ujenzi wa sekondari

Spread the loveBUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kukusanya fedha...

error: Content is protected !!