Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwinyi ataka Rais Magufuli aongezewe muda, yeye apinga
Habari za Siasa

Mwinyi ataka Rais Magufuli aongezewe muda, yeye apinga

Spread the love

ALI Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa awamu ya pili, ameshauri matumizi ya Katiba ya Tanzania yasitishwe kwa muda ili kumpa nafasi Rais John Magufuli, kuendelea kuongoza  nchi katika kipindi cha mpito. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Rais Mwinyi ametoa ushauri huo leo Jumamosi tarehe 11 Julai 2020, katika Mkutano Mkuu wa CCM, unaofanyika jijini Dodoma.

Rais Magufuli amechaguliwa tena na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), kugombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, ambapo anatafuta nafasi ya kumalizia muhula wake wa pili ili kukidhi matakwa ya Katiba ya Tanzania.

Hata hivyo, leo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wanapiga kura ya kumthibitisha Rais Magufuli kuwa mgombea wa urais wa chama hicho, katika uchaguzi huo.

Mwenyekiti huyo wa CCM alianza safari yake ya uongozi wa muhula wa kwanza tarehe 5 Novemba 2015, baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.

Akizungumza kwa niaba ya Marais wastaafu, Mwinyi amesema, licha ya kwamba Katiba ya Tanzania inapaswa kuenziwa, lakini kutokana na mambo mazuri aliyoyafanya Rais Magufuli, anatakiwa kuongezewa muhula mmoja, kama asante ya uongozi wake kwa Taifa.

“Nchi yetu ina katiba na katiba lazima tuienzi, tusiingilie lakini tukitaka tunaweza kuighairisha kwa muda mfupi ili kumpa rais wetu huyo kipindi kingine kimoja cha asante ,” amesema Rais Mwinyi.

Mwinyi amesema, Rais Magufuli amekuwa kiongozi wa mfano kutokana na kufanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ambayo wengine walishindwa kufanya.

“Sote tumeshuhudia toka umeingia rais wetu kafanya mengi makubwa mengine ya ajabu.  Sijasikia nchi isiyokuwa na hela kuweza kununua ndege 11 kwa pesa za ndani, sijasikia nchi masikini ikathubutu kushughulikia haya aliyoyashughulukia mengine nimeyasahau, “ amesema Mwinyi

“Mcheza kwao hutunzwa, ningetaka mambo mawili, kwa hakika kufikiriwa na hakika tuhakikishe tunashawishi Watanzania wenzetu rais wetu huyu apate matokeo mazuri,” amesema

Baada ya kumaliza, Rais Magufuli huku akifurahia alisema, Rais Mwinyi kwa nini marais wastaafu hawakuongeza muda, akiwemo yeye, Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete.

“Asante sana Mzee Mwinyi, mbona wewe hukukubali kuongeza siku zilizokuwa zimebaki?  Au Mzee Mkapa mbona hakuongeza? Lakini nimekuelewa wewe ni mtani wangu asante sana,” amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!