April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwingine apona corona Tanzania

Spread the love

MPAKA sasa, watu watatu wawaliokuwa wakisumbuliwa na ugonjwa wa corona, wamepona. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea)

Taarifa iliyotolewa na Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo tarehe 3 Aprili 2020, inaeleza kwamba mtu mmoja aliyekuwa na ugonjwa huo ameruhusiwa kuungana na familia yake baada ya kupona.

Mtu huyo anafanya idadi ya watu waliopona corona kufika watatu huku wengine 16 wakiendelea kupata matibabu. Kutokana na ugonjwa huyo, mto mmoja tayari ameripotiwa kufariki.

“Mgonjwa wa tatu aliyeambukizwa ugonjwa wa corona nchini, amepona na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Mgonjwa  mwingine mmoja kipimo cha pili kimeonesha hana tena virusi vya corona  hivyo anasubiri kipimo cha mwisho kuthibitishwa kupona,” amesema Waziri Ummy.

Amesema, mmoja wa wagonjwa hao ni yule aliyekuwa amelazwa kwenye kituo maalumu ya tiba cha  Mkoa wa Kagera, na kwamba mpaka sasa mkoa huo hauna mgonjwa.

“Arusha tulikuwa na wagonjwa wawili, mmoja aliruhusiwa na mgonjwa mwingine majibu ya leo asubuhi yameonesha kuwa ni ‘negative,’ (hana maambukizi) hivyo tunasubiri kipimo kingine kimoja ili aweze kuruhusiwa,” amesema Waziri Ummy.

Pia amewakumbusha wananchi kukaa mita moja au zaidi kati ya mtu mmoja na mtu mmoja ili kuweza kuzuia maambukizi mapya.

error: Content is protected !!