Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwili wa Mkapa warejeshwa hospitali ya Lugalo
Habari za Siasa

Mwili wa Mkapa warejeshwa hospitali ya Lugalo

Spread the love

MWILI wa Hayati Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa umerejeshwa Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kutoka Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mwili huo ulipelekwa uwanjani hapo mapema leo Jumapili tarehe 26 Julai 2020 kwa ajili ya misa ya kumuaga iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Tarcisius Ngalalekumtwa.

Baada ya kumalizika kwa misa hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wananchi na viongozi wakiongozwa na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, waombolezaji walipata fursa ya kuanza kuuaga.

Mwili huo umeondolewa uwanjani hapo saa 1:20 usiku.

Soma zaidi…

Serikali ya Tanzania imetangaza siku tatu za kuuaga mwili wa Rais huyo wa awamu ya tatu aliyeongoza Tanzania kuanzia mwaka 1995-2005 zitakazohitimishwa Jumanne tarehe 28 Julai 2020.

Safari yake ya mwisho hapa duniani, itahitimishwa Jumatano tarehe 29 Julai 2020 ambapo mwili wake utakapozikwa kijijini kwake, Lupaso, Masasi Mkoa wa Mtwara.

Kesho kuanzia asubuhi, mwili huo utapelekwa tena uwanjani hapo kwa ajili ya kuendelea kutoa fursa kwa watu mbalimbali kwenda kuuaga.

Mkapa alifikwa na mauti Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam kwa tatizo la mshituko wa moyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!