April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mweusi mwingine auawa Marekani

Spread the love

IKIWA ni zaidi ya wiki tatu ya maandamano kutokana na polisi wa Minnesota, Marekani kumuua raia mweusi wa taifa hilo George Floyd, tayari mauaji mengine ya kusudi yamefanyika nchini humo. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Rayshard Brooks (27), ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi Garrett Rolfe wa Jiji la Atlanta Ijumaa usiku jambo lililozidisha hasira kwa waandamanaji.

Taarifa zaidi zinaeleza, Brooks alipitiwa na usingizi kwenye eneo la kuegeshea magari nje ya Hoteli ya Wendy, jambo hilo lililosababisha gari zingine kushindwa kutoka kulingana na eneo ambalo gari lake lilipokuwa.

Polisi walipoitwa na kufika eneo hilo, walianza kumtolea maneno makali na vitisho jambo lililomfanya aanze kukimbia, ndipo alipopigwa risasi na kuuawa.

Polisi aliyefanya mauaji hayo, Rolfe tayari amefukuzwa kazi, hata hivyo Mkuu wa Polisi wa Atlanta, Erika Shields jana jumamosi tarehe 13 Juni 2020, amejiuzulu nafasi yake kutokana na mauaji hayo.

Rolfe aliajiriwa na jeshi hilo Oktoba 2013 ambapo nafasi yake Ukuu wa Kazi za Utawala Atlanta inashikiliwa na Devin Bronsan aliyeingia kwenye ajira Septemba 2018.

Mwanasheria wa familia ya Brooks, L. Chris Stewart amesema, polisi aliyemuua kijana huyo, lazima ashtakiwa kwa jinai, pia matumizi makubwa ya nguvu kwa mtu asiye na kitu chochote cha kujihami.

error: Content is protected !!