Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwandishi wa habari ajitosa Urais Zanzibar, wagombea wafika 29
Habari za Siasa

Mwandishi wa habari ajitosa Urais Zanzibar, wagombea wafika 29

Shaame Simai Mcha, akichukua fomu ya kinyang’anyiro cha Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Spread the love

SHAAME Simai Mcha ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, amejitosa katika kinyang’anyiro cha Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea)

Mcha amechukua fomu leo Alhamisi tarehe 25 Juni 2020, katika Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar na kuahidi endapo atapewa ridhaa ya kuwaongoza Wazanzibar, atahakikisha anaendeleza mazuri yaliyoanzishwa na Rais Ali Momahed Shein.

Amesema, ataimarisha uchumi kwa kuwekeza kwenye uvuvi ambao utatochea ajira kwa vijana.

“Nitaimarisha mapinduzi matukufu ya Zanzibar na Muungano wetu wa Tanzania,” amesema Mcha ambaye amekuwa mgombea wa 29 kuchukua fomu.

Pereira Ame Silima aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania

Mgombea huyo amesema, amefanya kazi maeneo mbalimbali na kwa sasa ni ofisa uhusiano wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kabla ya Mcha kuchukua fomu, ametanguliwa na Pereira Ame Silima aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuchukua fomu za kuwania Urais.

Mara baada ya kuchukua fomu, Silima amesema, Zanizbar kuna “tatizo kubwa sana na unyanyasaji la watoto na wananwake.”

“Hili limefanuyia kazi na kila aliyepita lakini matokeo hayajawa mazuri na mimi nikipita ridhaa nataka niweke mguu chini kuhakikisha tunapata ufumbuzi,” amesema.

Iddi Hamadi Iddi, akichukua fomu ya kinyang’anyiro cha Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Kwa upande wake, Iddi Hamadi Iddi amesema amejitosa kwenye mbio hizo ili kuwatumikia Wazanzibar kwani, “Urais ni dhamana, Urais siyo mapato, Urais siyo ukubwa mtu ni kushirikiana na wenzako kufuata Ilani, Katiba na miongozo ya Chama Cha Mapinduzi.”

Shughuli ya uchukuaji na urejeshaji fomu hizo ni kati ya tarehe 15 hadi 30 Juni 2020. Kati ya wagombea wote 29, wanawake ni watatu.

Wagombea wote 29 waliojitokeza ni;

  1. Mbwana Bakari Juma
  2. Balozi  Ali Abeid Karume
  3. Mbwana Yahya Mwinyi :
  4. Omar Sheha Mussa
  5. Dk. Hussein Ali Mwinyi
  6. Shamsi Vuai Nahodha
  7. Mohammed Jaffar Jumanne
  8. Mohammed Hijja Mohammed
  9. Issa Suleiman Nassor
  10. Profesa Makame Mnyaa Mabarawa
  11. Mwatum Mussa Sultan
  12. Haji Rashid Pandu
  13. Abdulhalim Mohammed Ali
  14. Jecha Salum Jecha
  15. Dk. Khalid Salum Mohammed
  16. Rashid Ali Juma
  17. Khamis Mussa Omar
  18. Mmanga Mjengo Mjawiri
  19. Hamad Yussuf Masauni
  20. Mohammed Aboud Mohammed
  21. Bakari  Rashid Bakari
  22. Hussein Ibrahim Makungu
  23. Ayoub Mohammed Mahmoud
  24. Hashim Salum Hashim
  25. Hasna Atai Masound
  26. Fatma Kombo Masound
  27. Iddi Hamadi Iddi
  28. Pereira Ame Silima
  29. Shaame Simai Mcha

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!