Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwanamke mwingine ajitosa  Urais Zanzibar
Habari za Siasa

Mwanamke mwingine ajitosa  Urais Zanzibar

Hasna Atai Masoud
Spread the love

HASNA Atai Masoud, amekuwa mwanamke wa pili kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Zanzibar, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Hasna amekabidhiwa fomu hiyo leo Jumatano tarehe 24 Juni 2020 katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, na Cassian Gallo’S, Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC, Idara ya Oganaizesheni  Zanzibar.

Mwatum Mussa Sultan ambaye kwa sasa yuko katika hatua za kutafuta wadhamini, alikuwa mwanamke wa kwanza kujitokeza katika kinyang’anyiro hicho, baada ya kuchukua fomu tarehe 19 Juni 2020.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Hasna mwenye miaka 40 amesema amejitokeza ili kuwatoa kimasomaso wanawake, pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Shein, anayemaliza muda wako.

“Rais wetu amejitahidi sana kuwainua na kuwapa nafasi mbalimbali wanawake za uongozi wa juu, mimi nikiwa miongoni mwao. Nimehamasika sana leo hii ndio maana nimesimama kuunga mkono juhudi za rais wangu,” amesema Hasna.

Akielezea wasifu wake, Hasna amesema ana Shahada ya Uzamili katika usimamizi wa biashara pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT).

Hasna amesema kwa sasa anafanya kazi kwenye Mamlaka ya Udhibiti na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia (ZPRA), kama Afisa wa Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ambako amehudumu kwa zaidi ya miaka 10.

Kada huyo wa CCM amesema, aliwahi kuwa Katibu wa Fedha na Uchumi katika Wadi ya Mkunazini visiwani Zanzibar.

Pia, aliwahi kugombea nafasi ya uwakilishi kupitia viti maalumu vya wasomi, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Hadi sasa takribani wanachama 25 wamechukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia CCM, tangu zoezi hilo lifunguliwe tarehe 15 Juni 2020.

Zoezi hilo linaloenda sambamba na utafutaji wadhamini 250 kwa kila mtia nia, linatarajiwa kufungwa tarehe 30 Juni 2020, ili kupisha vikao vya uteuzi, vitakavyoanza tarehe 6 hadi 12 Julai 2020.

Mchakato wa uteuzi utahitimishwa na Mkutano Mkuu wa CCM, utakaofanyika tarehe 11 na 12 Julai 2020, ambao utachagua jina moja la mgombea Urais Zanzibar.

Wengine 24 waliokwisha kuchukua fumo ni;

  1. Mbwana Bakari Juma
  2. Ali Abeid Karume
  3. Mbwana Yahya Mwinyi :
  4. Omar Sheha Mussa
  5. Hussein Ali Mwinyi
  6. Shamsi Vuai Nahodha
  7. Mohammed Jaffar Jumanne
  8. Mohammed Hijja Mohammed
  9. Issa Suleiman Nassor
  10. Makame Mnyaa Mabarawa
  11. Mwatum Mussa Sultan
  12. Haji Rashid Pandu
  13. Abdulhalim Mohammed Ali
  14. Jecha Salum Jecha
  15. Dk Khalid Salum Mohammed
  16. Rashid Ali Juma
  17. Khamis Mussa Omar
  18. Mmanga Mjengo Mjawiri
  19. Hamad Yussuf Masauni
  20. Mohammed Aboud Mohammed
  21. Bakari  Rashid Bakari
  22. Hussein Ibrahim Makungu
  23. Ayoub Mohammed Mahmoud
  24. Hashim Salum Hashim

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!