Tuesday , 19 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwanafunzi kidato cha nne mbaroni kwa kutupa kichanga
Habari Mchanganyiko

Mwanafunzi kidato cha nne mbaroni kwa kutupa kichanga

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei
Spread the love

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Isengo, Ines Mtundu (19) kwa kosa la kumtupa chooni mtoto mchanga. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 24 Septemba 2018 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei, inaeleza kuwa, mtuhumiwa alitenda tukio hilo jana wakati akiwa chooni saa chache baada ya kujifungua.

“Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 23.09.2018 majira ya saa 3:53 asubuhi huko maeneo ya Isengo – Airport ya zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa mjamzito na mara baada ya kujifungua chooni ndipo alimtupa mtoto huyo,” inaeleza taarifa ya Kamanda Matei.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, mara baada ya taarifa kulifikia Jeshi la Polisi, jitihada za haraka zilifanyika kwa kushirikiana na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na kufanikiwa kumuokoa mtoto mchanga akiwa hai.

“Mama na mtoto huyo wote wapo Hospitali ya Wazazi – Meta wakipatiwa matibabu. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani,” ianeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the loveSUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu,...

Habari Mchanganyiko

Bunge laja na Marathon kuchangia ujenzi wa sekondari

Spread the loveBUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kukusanya fedha...

error: Content is protected !!