January 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwamyeto atua Yanga, Niyonzima Azam

Spread the love

USAJILI wa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodamom Tanzania Bara kwa msimu ujao wa 2020/21 umeendelea kushika kasi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Mabingwa wa kihistoria, Timu ya Yanga imeendelea kuboresha ukuta wake kwa kumsajili beki kisiki wa Coastal Union ya Tanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, Bakari Nondo Mwamnyeto.

Mwamnyeto amehitimisha uvumi wa wapi anakwenda msimu ujao kwa kusaini mkataba wa miaka miwili ya kutumia timu ya wananchi.

Upande mwingine, timu ya Azam FC ya Dar es Salaam nayo imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa kimataifa wa Rwanda, Ally Niyonzima.

Niyonzima aliyekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga, amesaini kandarasi ya miaka miwili kama mchezaji huru.

Kiungo hiyo alikuwa akikipiga Rayon Sports ya Rwanda.

error: Content is protected !!