Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwambe ataka kuundwa Kamati ya Bunge kuchunguza ujenzi wa Viwanda  
Habari za SiasaTangulizi

Mwambe ataka kuundwa Kamati ya Bunge kuchunguza ujenzi wa Viwanda  

Spread the love

MBUNGE wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe, amemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuunda Kamati Maalum ya Bunge, ili kuchunguza utekelezaji wa sera ya serikali ya “taifa la viwanda.” Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Dodoma … (endelea).

Amesema, sera ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa taifa la viwanda, imeshindwa kutekelezeka, na kwamba viwanda vingi vinavyodaiwa vimejengwa, vimeishia kwenye makaratasi.

Alitoa kauli hiyo leo Jumatatu, tarehe 4 Februari 2019, bungeni mjini Dodoma. Alikuwa akichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji.

Taarifa ya kamati ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji, iliwasilishwa bungeni na mwenyekiti wake, mbunge wa Mvomero, Murad  Sadiq.

Akiongea kwa uchungu, Mwambe amesema, “mheshimiwa mwenyekiti, ninamuomba Spika wa Bunge, aunde Kamati Maalum ya Bunge ili kuchunguza, uwapo wa viwanda hivyo.”

Amesema, kwa ufahamu wake na kwa mujibu wa ripoti mbalimbali zilizoletwa bungeni na serikali na baadhi ya wadau, maelekezo ya Bunge kwa serikali, juu ya ujenzi wa viwanda hivyo, bado halijatekelezwa hata kwa asilimia tano.

Amesema, “serikali imekuwa ikihubiri kwa miaka mitatu mfululizo, kwamba inajenga viwanda na tayari kuna viwanda karibu elfu tatu vimefunguliwa. Lakini hakuna kitu. Taarifa ya Kamati na ile ya wadau wa viwanda, inaonyesha hakuna kilichofanyika. Ni porojo tupu.”

Kwa mujibu wa Mwambe, kuundwa kwa tume ya Bunge kutasaidia kuondoa upotoshaji wa idadi ya viwanda vilivyojengwa na vinavyofanya kazi.

Aidha, Mwambe amesema, Kamati Maalum ya Bunge itapata nafasi ya kuelekeza kwa ufasaha nini kifanyike ili kulifanya taifa kuwa la viwanda, katika muda huu mfupi wa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010.

Anasema, serikali imeshindwa kujenga viwanda kutokana na uhabwa wa fedha. Amesema, katika mwaka wa fedha uliyoisha (2017/2018), serikali ilitenga kiasi cha Sh. 200 bilioni kwenye maendeleo. Lakini imeweza kupeleka Sh. 800 milioni pekee.

“Hakuna kinachofanyika kwa sababu, hakuna fedha zinazopelekwa kwenye miradi ya maendeleo. Serikali imeendelea kuhubiri kisichotekelezeka. Ndio maana ninamtaka Spika Ndugai, aunde Kamati ya Bunge kuchunguza suala hili,” alisisitiza.

Akizungumzia kinachoitwa, “Sakata la Korosho,”  mbunge huyo machachari kutoka eneo la ukanda wa Kusini, ameituhumu serikali kwa hatua yake ya kuwanyang’anya wafanyabiashara wadogo korosho zao kwa kisingizio cha “Kang’omba.”

Amesema, Kangomba wapo kila sehemu. Kunzia kwenye korosho, alizeti hadi kwenye madini. Lakini serikali imeamua kutumia ubabe kuwanyang’anya Watanzania wenzao korosho zao kwa madai kuwa wanafanya magendo.

“Ninaitaka serikali kuwarejeshea mara moja wafanyabiashara wadogo wa korosho bidhaa zao. Hawa watu walikubaliana na wakulima. Kitendo cha serikali kuwanyang’anya korosho zao kwa kisingizio kuwa ni Kang’omba hakikubariki,” alisema Mwambe kwa sauti ya uchungu.

Hoja ya Mwambe ilimnyanyua Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, aliyedai kuwa wafanyabiashara hao walikuwa wanaendesha bishara zao, kinyume cha sheria.

Waziri Hasunga alisema, “Kangomba hawakusajiliwa. Kangomba wafanyabiashara haramu na hivyo serikali haiwezi kuwaruhusu kudhulumu wananchi.”

Ni kufuatia kauli hiyo ya waziri wa kilimo, ndipo Zitto Zuberi Kabwe, mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), alilieleza Bunge kuwa hata kwenye mazao ya pamba wamekuwa na utaratibu wa kuingia mikataba na wakulima hata mbegu za zao hilo kupandwa mashambani.

“Mheshimiwa mwenyekiti, naomba kuliarifu Bunge na kumjulisha mzungumzaji wa sasa (Cecil Mwambe), kwamba kwenye sekta ya pamba, wafanyabiashara wanaingia mikataba na wakulima kabla ya pamba kupandwa.”

Mwambe alikubaliana na taarifa ya Zitto na akarejea kauli yake ya kuitaka serikali kurejesha korosho za wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!