BARAZA Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema) kimependekeza kwa mkutano mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu kuwa mgombea mwenza wa urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)
Mwalimu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar amependekezwa leo Jumatatu tarehe 3 Agosti 2020 na kesho Jumanne atathibitishwa na mkutano mkuu.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa mkutano huo, Mwaimu ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari amesema, amejiandaa vyema kwenda kuhakikisha anapambana ili mgombea urais atangazwe baada ya uchaguzi kufanyika.
Mwalimu amesema yeye ni “mtoto wa Chadema ambaye sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote. Nimelelewa na chama hiki. Niko tayari kutumwa.”
Mwaimu amesema, jukumu hilo ni zito na matumaini yake, familia na watoto “wangu wananielewa kwani mgombea wetu kushinda atashinda ila kutangazwa tutahakikisha ametangazwa.”
Kura za wazi na wajumbe 456 zilipopigwa, watano walisema hapana na wengine ndio.
Leave a comment