Thursday , 25 April 2024
Habari MchanganyikoTangulizi

Mvua yatikisa Dar

Mkazi wa Tandale akiwa nje baada ya nyumba yake kuzingirwa na maji ya mvua
Spread the love

MVUA zinayoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam, zimesababisha uharibifu wa mali na makazi, maafa, madarasa ya shule kujaa maji na hata wanafunzi kurudishwa nyumbani. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mvua hizo zimeendelea kunyesha kwa siku tano mfululizo, kuanzia Jumapili ya tarehe 5 hadi leo tarehe 10 Mei 2019 ambapo mtu mmoja anaripotiwa kufariki.

Hassan Farihuna, aliyekuwa Mkazi wa Tandale kwa Mtogole wilayani Kinondoni amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumanne tarehe 7 Mei mwaka huu, baada ya nyumba yao kukumbwa na mafuriko.

Akizungumza kuhusu tukio hilo leo tarehe 10 Mei 2019, Bibi wa Marehemu Hassan, Bi Salma amesema, kijana wake alipoteza maisha katika mafuriko yaliyoikumba nyumba yake majira ya usiku.

“Majira ya saa saba usiku kipindi cha kula daku, aliporudi ndani alidondoka, tulivyomaliza kula chakula tukamkuta amepoteza maisha, tulimfikisha hospitalini wakasema mmetuletea mtu ameshakufa.  Sisi tulijua pengine amezimia,” amesema Bi Salma.

Bi. Salma amesema, kijana wake alizikwa tarehe 7 Mei mwaka huu kwenye makaburi ya Ali Maua, jijini Dar es Salaam.

Licha ya mvua hiyo kusababisha kifo cha Hassan, imeleta athari kwa wakazi wa Dar es Salaam kwa kuharibu mali.

Edina Mhando, Mkazi wa Tandale amesema, ameshindwa kufanya biashara zake kutokana na nyumba yake kuingiwa na mafuriko.

 Amesema, nyumba yake imekumbwa na mafuriko kutokana na ukuta uliojengwa mbele yake kwa ajili ya kuzuia maji yamafuriko, kubomolewa na wajenzi wa barabara ya Mtaa wa Kiboko Bar.

“Tuna matatizo ya hii barabara, tangu ujenzi umeanza hii nyumba imekuwa kero, wamekuja wakaangusha ukuta tukajaribu kufuatilia Wachina tuepukane na mafuriko wamekuwa wabishi,” amesema Edina na kuongeza;

“Wanatuahidi watakuja kutujengea mifereji lakini hawakuja wametuchimbia shimo hatimaye haya maji yameingia ndani, nyumba yote imeingia maji mpaka ndani, karibia wiki yoite sijafanya biashara.”

Elizabeth Gerald, Mjumbe wa Mtaa wa Kiboko Bar amesema, alijaribu kuwasiliana na viongozi wa ngazi za juu katika eneo hilo kuwagiza wakandarasi warekebishe ukuta huo, lakini jitihada zake hazikufua dafu.

“Tumekuja kujikinga huku, kule kwetu maji yamejaa kuna ukuta ulivunjika.  Tulitoa taarifa wakatuambia watakuja hawajaja, tokea Jumapili, tukitaka kulala tunapunguza maji ndio tunalala,” amesema Elizabeth.

Madarasa ya shule kadhaa yameingia maji kutokana na mvua hizo, miongoni mwa shule hizo ni pamoja na Shule ya Kiislam ya Answar iliyopo Kinondoni pamoja na Shule ya Msingi Msasani.

Mwalimu Edward Mollel, Mwalismu wa Shule ya Msingi Msasani amesema, wanafunzi waliohudhuria shuleni leo ni chini ya nusu ya wanafunzi wote wa shule hiyo na kwamba, darasa la kwanza na pili hawakufika kabisa.

Baadhi ya barabara ikiwemo ya Kawawa eneo la Bonde la Mkwajuni, maji yameathiri uendeshaji magari kutokana na kupita juu ya daraja hivyo kusababisha foleni ndefu.

Mamlaka ya Hali ha Hewa Tanzania (TMA) imeeleza kuwa, mwishoni mwa wiki, kunatarajiwa kuwepo mvua kubwa zaidi ya hizi zinazoendelea ambapo imewataka wananchi kuchukua tahadhari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!