Tuesday , 16 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mvua kubwa yatabiriwa Dar, Pwani
Habari Mchanganyiko

Mvua kubwa yatabiriwa Dar, Pwani

Mvua kubwa ikinyesha
Spread the love

MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini,( TMA) imetahadharisha ujio wa mvua kubwa kuanzia tarehe 23 Novemba 2018 hadi Aprili 2019, katika mikoa mbalimbali hasa Dar es Salaam na Pwani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). 

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 18 Oktoba 2018 na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Agnes Kijazi wakati akitoa utabiri huo kwa wanahabari jijini Dar es Salaam.

Kijazi ameeleza kuwa, mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Kusini mwa mkoa wa Morogoro, Lindi na Mtwara inatarajiwa kupata mvua za wastani na za juu ya wastani, wakati mikoa ya Rukwa, Katavi, Kigoma na Songea ikitarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Kufuatia utabiri huo, Kijazi amezitaka sekta mbalimbali zinazohusika na uchukuzi na mawasiliano, maji, nishati, mifugo na wanyamapori, usalama wa chakula na kilimo pamoja na afya, kuchukua tahadhari kufuatia mvua hizo ili kukwepa madhara yake.

“Mvua za msimu ni mahususi kwa maeneo ya magharibi mwa nchi, kanda ya kati, nyanda za juu kusini magharibi, kusini mwa nchi, ukanda wa pwani ya kusini pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro ambayo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka,” amesema Kijazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kamati ya bunge yapigia chapuo kilimo ikolojia

Spread the loveSERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeshauriwa kushirikiana na wadau wa...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Habari Mchanganyiko

Biashara kuanza kufanyika saa 24 Dar

Spread the loveUONGOZI wa Mkoa wa Dar es Salaam, unaendelea na vikao...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatakiwa kutunga sheria kudhibiti ajali mabasi ya shule

Spread the loveKUFUATIA ajali ya basi la shule ya msingi ya Ghati...

error: Content is protected !!