Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Muuguzi aliyebaka kutimuliwa  kazi 
Habari Mchanganyiko

Muuguzi aliyebaka kutimuliwa  kazi 

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Spread the love

SAKATA la  Muuguzi anayedaiwa kumbaka binti mwenye miaka 18 limeingia katika sura mpya, baada ya serikali kuingilia kati na kuomba Baraza la Wauguzi Tanzania kumsimamisha kazi mtumishi huyo, anaandika Hamisi Mguta.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeomba kusitishwa kwa muda leseni ya uuguzi na ukunga ya Damian Mguya baada ya kumbaka binti wa miaka 18.

Nsachris Mwamwacha, Msemaji wa Idara kuu ya Afya amesema kupitia taarifa yake kuwa muuguzi huyo alimbaka binti huyo baada ya kumdunga sindano ya usingizi.

“Uamuzi huo wa serikali umetokana na tuhuma za uvunjifu wa maadili ya taaluma kwa mujibu wa kifungu 13 (2) (c) na (d) ya (The Nursing and Midwifery act 2010),” amesema Mwamwacha.

Mguya (26) alishikiliwa na polisi wilayani Igunga, Tabora baada ya kufanya tukio hilo ambapo kwa mujibu wa Kamishna Wilbroad Mutafungwa, Kamanda wa Polisi mkoni humo alihojiwa na atafikishwa Mahakamani uchunguzi utakapokamilika.

Imeelezwa kuwa siku ya tukio msichana huyo alifika kwenye Zahanati kwa ajili ya kumuuguza Mama yake mzazi, ndipo muuguzi huyo alipotumia nafasi hiyo kumchoma sindano ya usingizi kisha kumbaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!