July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mutharika alia kupokwa ushindi

Peter Mutharika

Spread the love

CHAMA tawala cha Democratic Progressive Party (DPP), kinachoongozwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Peter Mutharika, kimelalamika kupokwa ushindi wake na chama cha upinzani cha Malawi Congress. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Francis Mphepo, katibu wa DPP amesema, tangu awali hawakuwa na imani na matokeo ya awali yaliyokuwa yakitangazwa na Uchaguzi ya Malawi (MEC), na kwamba aliomba kusimamishwa kwa matokeo hayo.  

Tayari Lazarus Chakwera, aliyekuwa mgombea wa chama cha upinzani cha DPP, ameapishwa kuwa rais wa taifa hilo baada ya kushinda kwa asilimia 58.57 katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.

“Hakuna shaka yoyote kwamba, vitendo vya udanganyifu vitaathiri matokeo kwa namna moja au nyengine,” amesema Mphepo.

Jumamosi iliyopita, Mutharika wa DPP alisema, ingawa hakubaliani na matokeo ya uchaguzi, ni imani yake kwamba nchi inastahili kusonga mbele.

Mapema hafla ya kumuapisha Chakwera kuwa rais mpya wa Malawi, ilifanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Lilongwe baada ya kiongozi huyo kushinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne wiki iliyopita.

Hata hivyo, Chakwera ambaye sasa ni rais mpya wa Malawi amesema, ushindi wake ni kama vile mtu aliyekufa kisha akafufuka.

Chakwera alitangazwa jana tarehe 28 Juni 2020, kwamba ameshinda kwa kupata asilimia 58.57 ya kura.

Lazarus Chakwera, Rais wa Malawi

“Sasa najiona kama Lazarus, naona nimefufuka baada ya kufa,” amesema Chakwera wakati akizungumza na mtandao wa habari wa BBC baada ya kuapishwa jana kuwa rais wa taifa hilo.

Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Malawi Congress amesema, matokeo aliyopata ni ushindi wa demokrasia na haki nchini humo.

Uchaguzi uliompa ushindi Lazarus ulifanika tarehe 23 Juni 2020 baada ya ule wa awali, uliofanyika Mei 2019, kufutwa na mahakama nchini humo Februari 2020 kutokana na kubainika kuwa na dosari.

Katika uchaguzi huo wa Mei 2019, Rais Mutharika alidaiwa kuibuka mshindi kwa kupata asilimia 38.57 huku Chakwera akipata asilimia 35.41.

Matokeo hayo yalisababisha kuibuka kwa vurugu, maandamano na shinikizo mbalimbali ambapo Chakwera alifungua kesi katika Mahakama ya Kikatiba kupinga matokeo hayo.

Hata hivyo, Februari 2020 mahakama hiyo ilifutilia mbali matokeo hayo ya awali na kuamuru uchaguzi kurudiwa.

Chakwera amesema, hata wale ambao hawako naye kwenye harakati zake za siasa, hawana sababu ya kugogopa baada yay eye kuibuka mshindi.

“Hakuna sababu ya kuhofu, nitakuwa rais wako na utaratibu wangu ni kufanya kazi na wote kwa kuwa tunajenga Malawi moja. Mimi sio rais wa kikundi, ni rais wa Wamalawi wote,” amesema Lazarus.

error: Content is protected !!