Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Muswada vyama vya siasa una vionjo vya ugaidi’
Habari za Siasa

‘Muswada vyama vya siasa una vionjo vya ugaidi’

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda Issa Ponda
Spread the love

MUUNDO wa Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa, uliowasilishwa bungeni na Serikali ya Jamhuri, unatajwa kusheheni vimelea vya sheria ya ugaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza mbele ya Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda Issa Ponda amesema, iwapo muswada huo utaachwa na kupita kama ulivyo, utaweza kuleta maafa kama ilivyo kwa sheria ya ugaidi. Jumuiya inaongoza zaidi ya taasisi 15 za kiislam nchini.

Sheikh Ponda anasema, maeneo mengi yaliyomo kwenye muswada, yamejikita katika kupoka uhuru wa wananchi ndani nan je ya vyama vyao.

Amesema, “kwa kuwa Muswada unalalamikiwa na wadau muhimu wa siasa na una vionjo kama vile vya sheria ya ugaidi, ni wazi ukipitishwa yatatokea maafa kupitia mlango wa siasa.”

Amesema, muswada wa ugaidi – kama ulivyo huu wa vyama vya siasa – ulilalamikiwa na makundi yote makubwa ya jamii wakiwamo wanasheria, wabunge, asasi za kijamii na kada zingine.

“Makundi hayo yalieleza wazi kuwa endapo muswada huo utapitishwa na kuwa sheria, taifa litatumbukia katika uvunjaji mkubwa wa haki za kikatiba na haki nyingine za kiraia. Matukio ya kukamatwa na kutekwa ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya ugaidi. Ndivyo hivyo sheria ya vyama inakoelekea,” ameeleza.

Katika maelezo yake yaliyopo kwenye ukurasa wa pili wa taarifa iliyowasilishwa, taasisi hizo zinasema, “marekebisho yanayotajwa kufanywa kwenye sheria hiyo ni makubwa kwa kiwango kinachostahili kuitwa Muswada Mpya wa Sheria ya Vyama vya Siasa.”

Kutokana na athari za muswada huo, Sheikh Ponda kupitia taasisi hizo, wameshauri kuwa muswada huo uondolewe bungeni.

Amesema, mara baada ya muswada huo kuondolewa, iundwe kamati ya kitaifa itakayopewa hadidu rejea kadhaa ikiwa ni pamoja na kupata maoni kutoka kwa wadau wote wa siasa, wananchi, taasisi za kijamii, mashirika ya dini na makundi mengine.

Aidha, Sheikh Ponda amependekeza kamati itakayoundwa iangalie mapungufu yaliyopo kwenye mfumo wa siasa nchini na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike.

Anasema, “tunaamini kwa namna hiyo, tunaweza kuwa tumetenda haki kuliko utaratibu huu unaotakiwa na serikali.”

Maoni ya Jumuiya hiyo yameeleza kuwa tayari wadau wameonesha udhaifu kwenye muswada huo; na kwamba endapo yataingizwa katika sheria ya vyama vya siasa, yataharibu kabisa mfumo wa siasa nchini.

“…haya yakipita, wananchi hawatakuwa na haja tena ya vyama vya siasa vilivyosajiliwa serikalini. Wananchi wanataka vyama vyao wenyewe, siyo vyama vya Jaji Mutungi,” ameeleza.

Amesema, “kwa vile harakati wanazozifanya kupitia vyama vya siasa ndizo huwawezesha kupata fursa ya kushiriki kuunda serikali, fursa ya kupaza sauti (wabunge) na kuingia katika uongozi wa taifa lao, watalazimika kuzifanya harakati hizo nje ya mfumo, ndio mfumo wa siasa uliopo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!