Yoweri Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda

Museveni kufanya ziara nchini

YOWERI Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini ifikapo tarehe 9 Agosti 2018. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo 07 Agosti 2018 na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

“Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Rais Museveni atapokelewa na mwenyeji wake Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema uliopo kati ya Tanzania na Uganda, ambapo Rais Museveni atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Rais Magufuli yatakayofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Rais Museveni na Ujumbe wake wataondoka nchini siku hiyo hiyo kurejea Uganda.

YOWERI Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini ifikapo tarehe 9 Agosti 2018. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea). Taarifa hiyo imetolewa leo 07 Agosti 2018 na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. “Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Rais Museveni atapokelewa na mwenyeji wake Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo. Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube