January 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Museveni achekwa na kamanda wake

Yoweri Museveni

Spread the love

JENERALI Mugisha Muntu, Kamanda wa zamani wa Jeshi la Uganda na aliyeshiriki kumweka madarakani Rais Yoweri Museveni mwaka 1986, sasa anamcheka. Unaripoti mtandao wa Daily Monitor…(endelea).

Amesema, Rais Museveni na serikali yake badala ya kukabiliana na chanzo cha maandamano nchini humo, serikali yake inakabiliana na waandamanaji.

Jenerali Muntu ambaye wakati huo alikuwa karibu na Rais Museveni amesema, serikali ya Museveni haipaswi kufunga milango ya majadiliano kuhusu usalama, amani, haki na usawa.

“Namna serikali inavyokabiliana na waandamanaji inachekesha, badala ya kukabiliana chanzo cha maandamano, wanakabiliana na waandamanaji,” amesema Jen. Muntu ambaye anagombea urais kupitia Chama cha Alliance for National Transformation (ANT).

Amesema, kama watu wanakandamizwa na kufikia hatua ya kutokuwa na kauli, wanachoweza kufanya ni kuingia kwenye mapambano.

Wiki iliyopita, maandamano yaliibuka katika miji mbalimbali nchini Uganda kutokana na kukamatwa kwa Robert Kyagulanyi (Bobi Wine), mgombea urais kupitia Chama cha National Unity.

Kwenye maandamano hayo, watu zaidi ya 45 wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa vibaya na hata kulazwa hospitali.

 

Amesema, vyama vya upinzani vimeingia kwenye mapambano naserikali kwa kuwa serikali imefunga milango ya majadiliano kuhusu haki, usawa na amani.

“Tumeamua kushika silaha kuvunja ukuta huo uliowekwa na serikali. Wenzetu walifariki wakati huo wa mapambano na wengine kama sisi tulibaki kwa majaliwa yake Mungu,” amesema Jen. Muntu.

Ameshauri kwamba, wakati wa makabidhiano ya madaraka kwa njia ya amani ni sasa kwa kuwa imeshindikana kufanya hivyo tangu Rais Museveni aingie madarakani.

Akizungumzia hisia za wanajeshi wa Uganda amesema, ni kama bomu linalosubiri kupasuka kwani wapo njia panda kutokana na utawala wa Museveni huku kukiwa na presha kubwa kutoka kwa vijana ambao wengi wao hawana ajira.

“Tunatakiwa tuingie kuongoza ili kuondoa sintofahamu iliyopo kwa sasa na kuijenga nchi upya,” amesema Jen. Muntu.

error: Content is protected !!