Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Muhimbili sasa kupandikiza ‘ujauzito’
Habari Mchanganyiko

Muhimbili sasa kupandikiza ‘ujauzito’

Spread the love

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imeweka mipango ya kuwa na huduma ya kupandikiza mbegu za ujauzito (mimba), ifikapo mwaka 2020. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 19 Novemba 2019, na Prof. Lawrence Museru, Mkurugenzi  Mtendaji wa hospitali hiyo.

Prof. Museru alikuwa akitoa taarifa kuhusu mafanikio ya  hospitali hiyo, kwa miaka minne ya serikali ya awamu ya tano.

Amesema, maboresho hayo yana lengo la kuhakikisha huduma zilizoanzishwa, zinatolewa katika mfumo endelevu.

Na kwamba, mainjinia wameanza kukarabati jengo katika hospitali hiyo, litakaloanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma hiyo, kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Mloganzila.

“Tumeishapeleka wataalamu nchini India, kuangalia namna ambavyo huduma ya upandikizaji mimba (IVF), inavyotolewa katika hospitali za umma.

“Ni miundombinu na vifaa gani vinahitajika, ununuzi wa vifaa unafanyika na mipango imeanza,” amesema.

Amesema, huduma hiyo itakuwa ya kulipia, “tutataka watu walipie, hatujajua itagharimu kiasi gani, hiyo ni mpaka wataalamu watakapofanya maamuzi.

“Lakini asiyeweza kulipia, tutaingia kwenye mfumo wa huduma za namna hiyo,” amesema.

Pia amesema, katika kipindi cha miaka hiyo mine, hospitali hiyo imetumia Sh 3.6 bilioni kusomesha wataalamu katika nchi mbalimbali, lengo likiwa kuwajengea uwezo ili kupunguza rufaa za matibabu nje ya nchi.

Amesema, zipo huduma ghali zilizokuwa zikitolewa nje ya nchi na sasa zinatilewa nchini kuwa ni pamoja na kupandikiza figo, vifaa vya usikivu, tiba radiolojia, tiba ya saratani ya damu, uchunguzi wa magonjwa ya mfumo wa chakula, ini na magonjwa mengine.

“Mwaka 2015 kero zilizokuwepo kwa wananchi ni vipimo kutofanya kazi kama MRI na CT-Scan kutokana na kuharibika kwa muda mrefu.

“Ukosefu wa dawa, wagonjwa waliokuwa wakilala chini kupewa vitanda, kulipa stahiki za wafanyakazi ikiwemo posho na nauli za likizo,” amesema.

Amesema, maendeleo na hatua zinazochukuliwa zimechangiwa na kauli ya Rais John Magufuli kutaka huduma bobezi zipatikane nchini.

“Rais Magufuli alitoa maagizo kuwa, Muhimbili ianze kutoa huduma za ubobezi ili kupunguza rufaa za nje ya nchi, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.

“Pia kununua na kukarabati vitendea kazi, na hapo ndipo tulianza kusomesha wataalamu ili kupunguza gharama,” amesema.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!