Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mtuhumiwa mkuu mauaji ya kimbari Rwanda akamatwa
Kimataifa

Mtuhumiwa mkuu mauaji ya kimbari Rwanda akamatwa

Félicien Kabuga
Spread the love

WIZARA ya sheria nchini Ufaransa, imetangaza kumkatama Félicien Kabuga, mmoja wa watuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda yaliyotokea mwaka 1994. Inaripoti mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili,  mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi mjini Asnières-Sur-Seine, eneo ambalo alikuwa anaishi kwa utambulisho wa uongo.

Mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda yamemshtaki, Kabuga mwenye umri wa miaka 84-kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Anadaiwa mfadhili mkuu wa wahutu ambao waliuwa watu 800,000 mwaka 1994.

Walikuwa wanawalenga kundi dogo la jamii ya Tutsi pamoja na wapinzani wao siasa.

Marekani ilitoa dau la dola 5 milioni kwa atakayeweza kutoa taarifa kuhusu, Kabuga ili aweze kukamatwa.

Mwendeshaji mkuu wa mashtaka wa kitengo cha mahakama ya Umoja Wa mataifa kwa ajili ya Rwanda-‘International Residual Mechanism for Criminal Tribunals’ (IRMCT) mjini Hague – mahakama inayosikiliza kesi za uhalifu wa vita za Rwanda na iliyokuwa Yugoslavia, alisema polisi wa Ufaransa walimkamata, Kabuga baada ya matokeo ya operesheni ya pamoja ya uchunguzi wa muda.

“Kukamatwa kwa, Félicien Kabuga leo hii inatukumbusha wale ambao walihusika katika mauaji ya kimbari kuwa wanapaswa kuwajibishwa hata kama ni baada ya miaka 26 baada ya uhalifu waliotenda,” Serge Brammertz alisema katika taarifa yake.

“Katika sheria za kimataifa, kukamatwa kwa Kabuga kunaonyesha kuwa tunaweza kufanikiwa kama tunakuwa na msaada ya kimataifa kukabiliana na hilo,” aliongeza.

Brammertz ameelezea shukrani zake kwa Ufaransa, lakini alisema hatua hii imefikiwa kwa mchango uliotolewa na Rwanda, Ubelgiji, Uingereza, Ujerumani, Uholanzi, Austria, Luxembourg, Uswizi, Marekani, Europol pamoja na Interpol.

Kufuatia taratibu ambazo ziko chini ya sheria ya Ufaransa, hukumu ya Kabuga inatarajiwa kuhamishwa kwenda kitengo cha mahakama ya Umoja wa mataifa kwa ajili ya Rwanda IRMCT, eneo ambalo kesi yake itasikilizwa.

Mwaka 1997, Kabuga alitajwa katika mahakama ya kimbari mara saba, kuhusika na mauaji ya kimbari, kwa kusuka mipango, kuua, kutishia kuua wakati wa kimbari.

Marekani ilisema, Kabuga alikuwa miongoni mwa waasisi na mwenyekiti wa chama cha Fonds de Défense Nationale (FDN), ingawa anadaiwa kutoa ufadhili kwa serikali ya Rwanda katika utekelezaji wa mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Alidaiwa pia kutoa msaada wa vifaa kwa wanamgambo waliofanya mauaji hayo kwa kuwapa silaha na sare na kuwapatia usafiri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!