Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mtu mweusi apigwa risasi Marekani, maandamano yaibuka
Kimataifa

Mtu mweusi apigwa risasi Marekani, maandamano yaibuka

Spread the love

MAANDAMANO yameibuka jimbo la Wisconsin nchini Marekani baada ya polisi kutuhumiwa kumpiga risasi mtu mweusi nchini humo, Jacob Blake. Inaripoti BBC…(endelea)

Video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha Blake akipigwa risasi kwa nyuma wakati anajaribu kuingia kwenye gari katika mji wa Kenosha.

Blake yupo hospitali akiendelea na matibabu huku mamlaka za Kenosha imetangaza hali ya dharura ya watu kutotoka nje baada ya kuzuka kwa maandamano.

Soma zaidi hapa

Mtu mweusi afanyiwa unyama Marekani

Mamia ya watu wameandamana hadi makao makuu ya polisi jana jumapili usiku na kuchoma moto magari huku waandamanaji wakipiga kelele wakisema hawawezi kurudi nyuma.

Tahadhari iliyotolewa kwa umma, polisi wamesema wanaofanya biashara saa 24 wafikirie kuzifunga kwasababu ya wizi na uvunjifu wa amani unaoweza kujitokeza.

Polisi wametumia mabomu ya machozi kutawanya mamia ya waandamanaji waliokiuka kauli ya kutotoka nje.
Gavana wa jimbo la Wisconsin, Tony Evers ameshutumu tukio hilo la kupigwa risasi Blake ambaye inasemekana hakuwa na silaha.

Evers amesema, wakati hana taarifa zote kwa sasa, anachojua ni kwamba huyo sio mtu wa kwanza kupigwa risasi au kujeruhiwa au kuuawa kiholela mikononi mwa polisi katika jimbo lao au nchi yao.

Idara ya haki ya Wisconsin inayochunguza tukio hilo, Imesema maafisa waliohusika wameagizwa kwenda likizo kwa uchunguzi zaidi.

Tukio hilo limetokea ikiwa imepitwa miezi michache tangu Afisa wa polisi mzungu kutuhumiwa kumuua raia wa Marekani, George Floyd.

Afisa huyo, Derek Chauvin aliyemkandamiza kwa mguu wake Floyd kisha kumfanya ashindwe kupumua na kupoteza maisha ameshtakiwa kwa mauaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!