Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mtoto wa Lowassa ajitosa ubunge Monduli
Habari za Siasa

Mtoto wa Lowassa ajitosa ubunge Monduli

Spread the love

FREDRICK, mtoto wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amechukua fomu ya kugombea ubunge Monduli, mkoani Arusha kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Fredrick amechukua fomu hiyo leo Jumanne tarehe 14 Julai 2020, katika Ofisi za CCM wilayani Monduli, mkoani Arusha na kukabidhiwa na Katibu wa chama hicho Wilaya ya Monduli, Langael Akyoo.

Mtoto huyo wa Lowassa amechukua fomu hiyo ili kujaribu bahati ya kuliongoza jimbo hilo, lililokuwa mikononi mwa baba yake tangu mwaka 1990 hadi 2015.

Lowassa aliliongoza jimbo hilo katika vipindi vitano mfululizo, kupitia Chama cha CCM.

Mwaka 2015 baada ya kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na kugombea urais na kuungwa mkono na vyama vya CUF, NLD na NCCR-Mageuzi vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), jimbo hilo lilikwenda upinzani.

Julius Kalanga alishinda ubunge kupitia Chadema. Hata hivyo,  usiku wa tarehe 31 Julai 2018 alijiuzulu ubunge na kuhamia CCM ambako alipitishwa tena kuwania ubunge na kushinda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!