Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mtemvu aongoza Kibamba, Vicky Kamata aanguka
Habari za Siasa

Mtemvu aongoza Kibamba, Vicky Kamata aanguka

Spread the love

ISSA Mtemvu, ameibuka mshindi kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Kibamba, Dar es Salaam kwa kupata kura 83 kati ya 369. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mkutano wa kura za maoni umefanyika leo Jumanne tarehe 21 Julai 2020 katika ukumbi wa Victorius Genesis, Kimara Temboni, Dar es Salaam.

Issa ni mdogo wake na Abbas Mtemvu ambaye naye ameongoza kura za maoni jimbo la Temeke, Dar es Salaam.

Katika matokeo hayo ya Kibamba, Vicky Kamata, Mbunge Viti Maalum anayemaliza muda wake, ameshika nafasi ya pili akipata kura 49 huku Mwesigwa Siraji akishika nafasi ya tatu kwa kura 36.

Wagombea waliochukua fomu walikuwa 176 lakini waliorejesha walikuwa 170 ambao wote kwa pamoja walijinadi kwa wajumbe wa mkutano huo ili waweze kuwapigia kura.

Katika hatua nyingine, Mbunge anayemaliza muda wake wa Kalenda Mkoa wa Iringa, Godfrey Mgimwa ameshindwa kura za maoni kwa kupata kura saba.

Aliyoongoza ni Jackson Kiswaga aliyepata kura 221 akifuatiwa na Leo Martin Mavika kura 149 na Bryson Kibasa kura 33. Wapiga kura walikuwa 589.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!