Julius Mtatiro, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru

Mtatiro aagiza AMCOS Ruvuma vichunguzwe

JULIUS Mtatiro, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuchunguza Vyama vya Ushirika vya Mazao (AMCOS), juu ya matumizi mabaya ya fedha za mauzo ya zao la korosho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma … (endelea).

Mtatiro ametoa agizo hilo jana tarehe 20 Februari 2020, wakati akifungua mafunzo ya vyama hivyo na vyama vya akiba na mikopo, mkoani Ruvuma.

Kiongozi huyo wa wilaya ya Tunduru amedai kwmaba, kuna baadhi ya viongozi wa AMCOS wanatumia fedha za korosho kutoa rushwa, ili wapitishwe katika uchaguzi wa vyama hivyo, unaotarajia kufanyika hivi karibuni.

Mtatiro amedai kuwa, baada ya uchaguzi wa AMCOS kutangazwa, viongozi wa vyama hivyo wasio waadilifu, wameanza kupitisha fedha.

“Serikali iko makini, kwa uzoefu wangu nimeupata kwenye msimu huu wa korosho unanitosha kabisa kuanza kujua nini kinaendelea kwenye korosho. Umetangazwa uchaguzi watu wnaanza kupitisha hela kwenye AMCOS na nimeshawaambia TAKUKURU waanze kazi yao na tunawajua,” amedai Mtatiro na kuongeza:

“Ttunajua hela zinatoka wapi na katika uchaguzi watu ndio wanaanza kuweka hela kwenye AMCOS mimi sina maslahi kwenye korosho nitasimama upande wa wakulima viongozi na watendaji wanaotumia maadili kuhakikisha mazao haya yanaleta tija kwa wakulima.”

Mtatiro amewaonya vigogo wa AMCOS wanaoshiriki uchaguzi huo  kutofanya vitendo vya kuhujumu watu wengine wasishiriki uchaguzo huo.

“Zoezi la uchaguzi la mwaka huu ni makini sisi tunaratibu, tunajua wapi tutakukuta. Utakeleta choko choko sisi tutamshuhulikia, acheni watu wachukue fomu wao ambao hawataki kupumzika waache. Pangeni jichagueni peke yenu, pingeni wengine wasichukue fomu, kuna wengine wanasema nikitolewa kwenye AMCOS yangu hakutakalika, kusikalike? tuna njia nyingi tutakushughulikia,” ameonya Mtatiro.

JULIUS Mtatiro, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuchunguza Vyama vya Ushirika vya Mazao (AMCOS), juu ya matumizi mabaya ya fedha za mauzo ya zao la korosho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma … (endelea). Mtatiro ametoa agizo hilo jana tarehe 20 Februari 2020, wakati akifungua mafunzo ya vyama hivyo na vyama vya akiba na mikopo, mkoani Ruvuma. Kiongozi huyo wa wilaya ya Tunduru amedai kwmaba, kuna baadhi ya viongozi wa AMCOS wanatumia fedha za korosho kutoa rushwa, ili wapitishwe katika uchaguzi wa vyama hivyo, unaotarajia kufanyika hivi karibuni. Mtatiro amedai kuwa,…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram