Tuesday , 19 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Mtandao wa Wanafunzi waipongeza TCU
Elimu

Mtandao wa Wanafunzi waipongeza TCU

Alphonce Lusako, ofisa wa ukaguzi wa haki za binaadamu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). Picha ndogo Hellen Sisya, Ofisa Habari wa TSNP
Spread the love

MTANDAO wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) umetoa shukrani kwa Tume ya Vyuo Vikuu  (TCU) kwa kukubali ushauri wao wa utaratibu mpya wa wanafunzi wa elimu ya juu wa kujithibitishia vyuo au programu wanazotaka kusoma. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Kupitia barua iliyotolewa leo na Afisa Habari wa TSNP, Heleen Sisya barua hiyo inasomeka kama ifuatavyo…

Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP), unapenda kuwataarifu wanafunzi na umma kuwa tarehe 20 Julai 2018, dirisha la udahili lilifunguliwa kwa wanafunzi wa kidato cha sita kuomba vyuo hadi hapo kesho kutwa tar 15 Agosti 2018.

Inakumbukwa kuwa udahili wa mwaka jana 2017, ulikuwa na changamoto kubwa ya Chuo kumthibitishia mwanafunzi ikaleta usumbufu mkubwa kwani vyuo baadhi vilikuwa vikiwathibitishia wanafunzi vyuo ambavyo wao hawajadhibitisha jambo ambalo lilileta usumbufu mkubwa hadi katika ugawaji wa Mikopo elimu ya juu kwani wanafunzi wengi walionekana katika kundi la waliodahiliwa vyuo zaidi ya kimoja.

Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP), katika kulishughulikia hili, tarehe 6 Juni 2018, tuliandikia barua TCU na nakala tukapeleka wizara ya elimu Dodoma kushauri ibadili mfumo wa kuthibitisha chuo kwa wawanafunzi isiwape mamlaka moja kwa moja chuo kwani kuna vyuo vilikuwa vikiwathibitishia wanafunzi badala ya mwanafunzi mwenyewe kujithibitishia chuo anachopenda kwenda na TSNP tumekuwa tukipigia kelele sana changamoto hii.

Tarehe 11 Juni /l2018, Mtandao wa wanafunzi tulipokea majibu kutoka kwa katibu mtendaji wa tume ya vyuo vikuu TCU ,yenye kumb.Na:CA.6/283/01L/47 akitujulisha kupokea changamoto zetu na akaahidi kuzifanyia kazi.

Leo tarehe 14, tumesikia taarifa ya katibu mtendaji tume ya vyuo vikuu akitambulisha utaratibu mpya wa kuthibitisha, ili kuthibitisha mwanafunzi atatumiwa namba ya siri ambayo atakuwa akiingiza katika chuo alichopenda kwenda kati ya ambavyo atakuwa amechaguliwa, hii ndio itakuwa njia mpya ya kuthibitisha.

Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) tunapenda kupongeza tume ya vyuo vikuu ,kwa weledi wao wa kupokea mapendekezo na kuyafanyia kazi, hakika hii ndio njia bora ambayo Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) tumekuwa tukipenda itumike, kwani itaepusha vyuo visivyo na uaminifu kuthibitishia kwani namba hiyo ya siri ya kuthibitisha itakuwa moja na itatolewa kwa muhusika hivyo mamlaka ya kuthibitisha yatakuwa kwa mwanafunzi mwenyewe.

Mungu awabariki sana, Mungu awaongoze Tume ya vyuo vikuu TCU, Tunawatakia majukumu mema.

Imetolewa na;
Hellen Sisya
Afisa Habari (TSNP)

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

RC Songwe ang’aka kesi 2 kati ya 60 za mafataki kuamuliwa

Spread the loveMkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael ameshangazwa na...

Elimu

Takukuru wambana Mwalimu mkuu, atema bungo

Spread the loveMwalimu Mkuu wa shule msingi Hanihani, kata ya Igunga wilayani...

error: Content is protected !!