Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msikiti UDOM ‘wawakutanisha’ Sheikh Ponda, Rais Magufuli
Habari za Siasa

Msikiti UDOM ‘wawakutanisha’ Sheikh Ponda, Rais Magufuli

Spread the love

SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini ametaka hatua stahiki zichukuliwe kwa walioshiriki kuvunja msikiti katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Amesema, kitendo cha uvunjwaji msikiti huo kinaleta taswira mbaya kwa nchi na kwamba, juhudi za hisia za kidini zinapaswa kukomeshwa kwa maslahi ya nchi.

Hivi karibuni Rais John Magufuli mbele ya viongozi wa dini alisema, kadhia ya uvunjwaji msikiti huo itashughulikiwa.

Alikwenda mbali kwa kueleza ‘ni utaratibu wa kawaida vyuo kuwa na maeneo ya ibada.’

Sheikh Ponda amesema, kitendo cha uvunjaji msikiti huo  kina viashiria vya ubaguzi na kuwa serikali inapaswa kufanya juhudi kuzuia hisia hizo hasi kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Amesema, fikra hasi pia zinatokana na uongozi chuo hicho kuwahamisha watumishi na wahadhiri 11 wa chuo hicho jambo ambalo linaakisi kumea kwa hisia za kidini.

“Lazima fikra hasi ziibuke, watumishi hao wote waliohamishwa ni Waislam,” amesema Sheikh Ponda na kuongeza;

“Asubuhi ya tarehe 9 Januari 2019 Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Peter Msoffe  alisitisha Ujenzi wa Msikiti kwa kile alichodai kuwa, amepata maagizo kutoka kwa Mwenyekiti aa Baraza la Chuo Gaudensia Kabaka.”

Amesema, tarehe 11 Januari 2019 wahadhiri na watumishi 11 waliokuwa wakishughulikia kwa karibu ujenzi wa msikiti huo walihamishwa kitu ambacho kimeshangaza.

“Kuhamisha wafanyakazi ni jambo la kawaida lakini angalia mazingira ya tukio na imani ya watu walioondolewa chuoni hapo,” amesema.

Amesema, Rais Magufuli alifikishiwa kadhia hiyo lakini hakuzungumiza hatua yoyote juu ya  watumishi waliotekeleza uhalifu huo.

“Kitendo hiko kina kwazo juhudi za Serikali na dini kwenye kujenga maadili . Kwani moja ya tatizo kwenye nchi yetu watu kutojengwa kimaadili” amesema.

Pamoja na kulaani kitendo hicho Sheikh Ponda amesema kuwa, tukio hilo ni sawa  a lile la mwaka 2012 Mbagala kwa raia 10 waliofungwa  mwaka mmoja gerezani kwa kuvunja Kanisa.

Pia amesema, tukio hilo ni sawa na lile la Kagera la raia wawili waliofungwa maisha jela kwa kuchoma moto kanisa.

Sheikh Ponda ameiombaa serikali kuwawajibisha kisheria watu hao pamoja na kuruhusu ujunzi wa msikiti huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!