Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msiba wa Ruge wakwamisha kesi ya Halima Mdee
Habari za SiasaTangulizi

Msiba wa Ruge wakwamisha kesi ya Halima Mdee

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha usikilizaji wa kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, kufuatia shahidi wa upande wa mashitaka kushindwa kufika mahakamani. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Wakili wa Serikali, Ashura Mzava ameiambia mahakama kuwa shahidi huyo ameshindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi wake, kutokana na msiba wa bosi wake, Ruge Mutahaba. 

Shahidi aliyeshindwa kufika Mahakamani, ni Abdul Mchembea, mfanyakazi wa Clouds Media Group Limited (CMG). Amefiwa na bosi wake – mkurugenzi wa matangazo -aliyefariki dunia juzi tarehe 26 Februari 2019, nchini Afrika Kusini.

Taarifa zinasema, Ruge alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya ini na figo.

Kesi hiyo ambayo iko mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Hakimu Simba amesema, kutokana na dharura hiyo kesi imeahirishwa mapaka tarehe 21 Machi mwaka huu.

Mdee anadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 3 Julai 2017 akiwa makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Mdee anatuhumiwa kutamka maneno kuwa “anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afunge breki;” na kwamba kitendo hicho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!