Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya MSD yawatangazia ‘neema’ wagonjwa
Afya

MSD yawatangazia ‘neema’ wagonjwa

Spread the love

BOHARI ya Dawa hapa nchini (MSD) leo imetangaza hali ya kuridhisha ya upatikanaji wa dawa na kusema hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu aina 17 ya dawa zitawasili kwamba upatikanaji wa dawa unategemewa kuwa asilimia 86, anaandika Pendo Omary.

Laurean Rugambwa, Mkurugenzi Mkuu – MSD leo amewaambia waandishi wa habari kwamba, “hadi kufikia Februari mwaka huu aiana tatu za dawa zitawasili na hali ya upatikanaji wa dawa inategemewa kuwa asilimia 88.” 

“Vilevile hadi kufikia mwezi Machi 2017 tunatarajia aina mbili za dawa zitawasili na hali ya upatikanaji wa dawa inategemewa kufikia asilimia 90 na hivyo kuwepo kwa aina 100 za dawa kati ya 135 ya dawa zote muhimu,” amesema Rugambwa.

Rugambwa amesema kwa upande wa dawa za miradi Msonge ambazo zinatibu na kuzuia magojwa ya Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu, Ukoma, Kichaa cha Mbwa, uzazi wa mpango na chanjo mbalimbali dawa hizo zipo kwa asilimia 100.

Itakumbukwa kuwa, mwishoni mwa mwaka jana taarifa iliyotolewa na taasisi isiyo ya kiserikali inayofuatiiia masuala ya Afya inayojulikana kwa jina la Sikika ilisema kuwa MSD inakabiliwa na upungufu wa dawa na kueleza kuwa kuna makopo 173 tu ya dawa aina ya Paracetamol nchini.

Taarifa hiyo iliungwa mkono na baadhi ya wananchi wakiwemo waonjwa katika wilaya mbalimbali hapa nchini walioeleza kuwa upatikanaji wa dawa na chanjo kwa watoto ulikuwa mgumu. Taarifa ambazo zilikuwa zikikanushwa vikali na Wizara ya Afya.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!