JAJI Francis Katabazi Mutungi, ameonywa kutojilimbikizia madaraka na kutaka kujiwekea kinga ya kutoshitakiwa mahakamani wakati yeye amebeba roho ya umma. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Onyo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Vicenti Mashinji, mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, mjini Dodoma.
Taarifa kutoka ndani ya kamati hiyo, zinaeleza kuwa chama hicho kimedai kuwa mapendekezo yaliyomo kwenye baadhi ya vifungu vya muswada, “yanampa Msajili mamlaka ya Kiungu.”
“Hapa kuna hila. Hakuna hiyo nia njema inayotajwa. Ndio maana msajili anahofia kupelekwa mahakamani. Kama angekuwa anaongozwa na dhamira njema, hili lisingekuwapo. Ndio maana anataka kinga. Nadhani kuna jambo baya ambalo analitaka kulifanya,” ameeleza Dk. Mashinji.
Amesema, “ni bahati mbaya sana, kwamba sheria hii inasimamiwa na msajili ambaye ni jaji wa Mahakama Kuu. Hatua ya Jaji kuogopa mahakama, kunathibitisha kuwa kuna nia ovu.”
Tangu kuwasilishwa bungeni muswada wa sheria ya vyama vya siasa, kumeibuka malumbano makali kati ya viongozi wa vyama vya upinzani na wale wanaotoka chama tawala.
Leave a comment