Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Msafara wa Kigwangalla wapata ajali, mmoja afariki
Habari MchanganyikoTangulizi

Msafara wa Kigwangalla wapata ajali, mmoja afariki

Spread the love

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amepata ajali alfajiri ya leo tarehe 4 Agosti, 2018 kwenye eneo la Magugu mkoani Manyara akiwa safarini akitokeaArusha kuelekea Dodoma. Anaripoti Regina Kelvin…(endelea).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema Afisa wa Habari wa Wizara hiyo, Hamza Temba aliyekuwa kwenye msafara wa waziri amefariki dunia.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, RPC Ramadhan Ng’azi Rpc amethibitisha taarifa za ajali hiyo ambapo amesema Waziri Kigwangalla amepata ajali hiyo Mkoani Manyara alipokuwa njiani akitokea Arusha kuelekea Dodoma.

“Ajali alipata mkoani Manyara, alikuwa Arusha kikazi akaondoka alfajiri kuelekea safari yake nafikiri Dodoma alipofika Manyara tukapewa taarifa kwamba amepata ajali,” amesema RPC Ng’azi.

Taarifa zinasema Dk. Kigangwalla anaendelea vizuri na anapelekwa hospitali ya Mount meru Arusha pamoja na msaidizi wake ambaye ameumia sana kwa kutumia helkopta kutoka Magugu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

error: Content is protected !!