Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mrisho Gambo alivyompongeza mrithi wake Arusha
Habari za Siasa

Mrisho Gambo alivyompongeza mrithi wake Arusha

Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini (CCM)
Spread the love

MRISHO Gambo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ametoa pongezi kwa mrithi wake, Iddy Kimanta katika nafasi hiyo na kumwomba Mungu akamsimamie kwenye utumishi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Gambo alitoa kauli jana Jumatatu tarehe 22 Juni 2020, muda mfupi kupita baada ya Rais John Magufuli kumwapisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha hafla iliyofanyikia Ikulu ya Dar es Salaam.

Uteuzi wa Gambo ulitenguliwa Ijumaa iliyopita tarehe 19 Juni 2020 na Rais Magufuli kumteua Kimanta ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli mkoani humo.

Gambo alitumia akaunti yake ya Instagram kutoa pongezi hizo akiambatanisha na picha ya Kimanta akiapishwa akisema, “Hongera sana Mzee wangu Iddy Kimanta Kwa kuteuliwa na kuapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Nakutakia kila la heri na Mungu akakusimamie kwenye kazi zako. Rais Magufuli kafanya mambo mengi na makubwa Arusha.”

Gambo aliongoza Mkoa wa Arusha kuanzia tarehe 18 Agosti 2016 akichukua nafasi ya Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Mbali na Gambo, wengine waliotenguliwa pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha(DC), Gabriel Daqarro ambaye nafasi yake alimteua Kenan Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, Kihongosi alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa.

Pia, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Arusha (DED) Dk. Maulid Madeni na kumteua Dk. John Pima kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, Dk.Pima alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.

Aidha, Rais Magufuli alimteua, Jerry Mwaga kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.

Kabla ya uteuzi huo, Mwaga alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wote hao waliapishwa jana Jumatatu Ikulu ya Dar es Salaam.

Rais Magufuli alisema, amewatengua viongozi hao baada ya kutokuelewana katika majukumu yao kwa zaidi ya miaka miwili. Pia, aliwataka wateule wake kufanya kazi kwa ushirikiano kwa mkubwa kumheshimu mdogo na mdogo kumheshimu mkubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!