Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mpango wa amani Afghanstan wapita pagumu
Kimataifa

Mpango wa amani Afghanstan wapita pagumu

Spread the love

ZALMAY Khalilzad, mjumbe wa Marekani katika kutafuta amani nchini Afghanstan, bado anatetea uamuzi wa kuwachia huru maelfu ya wafungwa wa Talban, ingawa bado “hafurahii na utekelezaji wa makubalino yaliyofikiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema, “…hakuna namna. Ilitubidi kufanya maamuzi magumu, ili kufikia malengo ya kupatikana amani iliyopotea kwa miaka 19 iliyopita.”

Akizungumza na shirika la habari la Uingereza (BBC), Khalilzad alisema, “hakuna ushahidi wowote kuwa baadhi ya wafungwa walioachiwa huru, wamerejea katika mapigano.”

Kiongozi huyo wa mazungumzo ya amani ya Alikuwa akijibu madai kuwa baadhi ya wafungwa waliokuwa gerezani na ambao wameachiwa huru kufuatia makubaliano hayo, wameamua kurejea msituni.

Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya kuwa na mazungumzo ya amani na kundi la wanamgambo wa kiislamu.

Marekani na kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Talban walifanya mazungumzo ya amani mwishoni mwa mwaka jana mjini Qatar, bila kuhusisha Afghanistan.

Katika mazungumzo hayo, Marekani ilikubali kushinikiza Afghanistan ili kuwachia huru wafungwa 5,000 wa Talban, ili kumaliza mapigano yaliyodumu kwa miaka 19 sasa.

Kuachiwa huru kwa wafungwa 5,000 lilikuwa sharti walilokubaliana Marekani na Taliban baada ya mazungumzo ya amani ya mwaka jana yaliyozaa mazungumzo haya.

Serikali ya Afghanistan haikuhusishwa katika kuweka makubaliano hayo na wana wasiwasi kuhusu kuachiwa huru kwa maelfu ya wanamgambo hao wa Taliban.

Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani, amenukuliwa na  Shirika la habari la Ufaransa (AFP), mwezi uliyopita akisema, “kuachiwa huru kwa wafungwa ni jambo hatari duniani.”

“Hatupingi mpango wa amani. Tunaupenda. Lakini tulitamani kuufikia mpango wa amani, lakini si kwa gharama hiyo,” Bwana Ghani alieleza.

Hata hivyo, Bwana Khalilzad amekataa madai kuwa kuachiwa huru kwa wafungwa wengi kiasi hicho, baadhi yao wakiwa ni watu hatari sana, “lilikuwa ni kosa.”

“Ninathamini jitihada walizozifanya serikali. Ninawapongeza kwa kufanya maamuzi magumu. Ni kupitia maamuzi hayo tumeweza kusababisha kuwapo kwa mazungumzo haya ya ana kwa ana ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza, tangu kuanza mapigano haya miaka 19 iliyopita,” alisisitiza.

Taliban iliondolewa madarakani nchini Afghanistan na jeshi la Marekani tarehe 7 Oktoba 2001, kufuatia mashambulizi ya Septemba 11 yaliodaiwa kufanywa na kundi la Al-Qaeda.

Tangu wakati huo, kundi hilo limepata nguvu ya kudhibiti maeneo mengine na kuendelea kung’ang’aniza madai kuwa bila kuondolewa kabisa kwa majeshi yote ya kigeni nchini Afghanistan, hakuna amani ya kudumu itakayopatikana.

Lakini kufikia mwaka 2003, Marekani ilihamishia nguvu zake nchini Iraq.

Hatua ya Marekani kuwekeza Iraq, kukaipa nafasi Taliban na makundi mengine ya Kiislamu kurudi nyuma kwenye ngome zao kusini na mashariki mwa Afghanistan, kuanza kujipanga upya na hatimaye kuweza kusafiri kwa urahisi kwenda na kutoka eneo la Pakistan lenye mamlaka yake ya ndani.

Februari 2007 waasi wa Taliban walishambulia kituo cha jeshi la Marekani nchini Afghanistan, wakati makamu wa rais Dick Cheney akiwa ziarani nchini humo, na kuuwa 24.

Rais wa Marekani Barack Obama aliamuru kuongezwa wanajeshi 30,000 zaidi nchini Afghanistan Desemba 2009, lakini akasema uondoaji utaanza Julai 2011. Idadi ya wanajeshi wa jumuiya ya kujihami ya NATO ikaongezeka na kufikia kilele cha wanajeshi 150,000 katika msimu wa joto mwaka 2010.

Hatimaye Mei 2011 kiongozi wa kundi la Al-Qaeda, Osama bin Laden alidaiwa kuuawa na vikosi maalumu vya Marekani nchini Pakistan.

Mauaji hayo yakapelekea miito ya kukomeshwa kwa vita hivyo. Muda mfupi baadae, Obama alitangaza kwamba wanajeshi 33,000 wa Marekani wataondolewa kufikia katikati ya mwaka 2012.

Lakini matumaini ya mazungumzo yalififia wakati Burhanuddin Rabbani – Rais wa zamani na wakati huo akiwa mjumbe wa amani wa Rais Hamid Karzai – alipouawa  na kuwa mwanasiasa wa kwanza wa juu zaidi kuuawa katika mgogoro huo, katika mauaji ya Septemba 2011 ambayo maafisa wa serikali ya Afghanistan walilaumu kundi la Taliban.

Juni 2013, Taliban walifungua ofisi nchini Qatar, kufuatia majadiliano ya siri na maafisa wa Marekani katika hatua ya kwanza kuelekea uwezekano wa makubaliano ya amani. Lakini mkakati huo ulivunjika mwezi mmoja baadae, baada ya ofisi hiyo kumkasirisha Karzai kwa kujitaja kuwa ubalozi usiyo rasmi wa serikali ilioko uhamishoni.

Desemba 2014, NATO ilihitimisha rasmi ujumbe wake wa mapambano nchini Afghanistan, na kukabidhi jukumu la kulinda usalama kwa vikosi dhaifu vya Afghanistan vilivyokuwa vinakabiliana na idadi inayoongezeka ya vifo na utoro.

Lakini matumaini yakaongezeka tena wakati mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Kabul na Wataliban wa Afghanistan – ya kwanza ya mgogoro huo – yalipoanza  nchini Pakistan Julai 2015.

Ufichuzi wa kushtua kwamba Mullah Omar, mwasisi wa Taliban, alikuwa amefariki miaka miwili iliopita, na kwamba kundi hilo lilificha kifo chake, ukakwamisha haraka mazungumzo hayo.

Katika mwaka uliofuata, hali ya usalama ilizorota nchini Afghanistan, hasa mjini Kabul, huku kundi changa la dola la Kiislamu likiongezea changamoto zinazovikabili vikosi vya usalama vya serikali. Mji huo mkuu ukageuka eneo hatari zaidi kwa maisha ya raia wakati idadi ya wahanga ikizidi kupanda.

Mwezi Februari mwaka huu wa 2018, Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani alizindua mpango wa kuanzisha mazungumzo na Taliban, ikiwemo hatimaye kulitambua kama chama cha siasa. Alipendekeza usitishaji mapigano kama sehemu ya mpango huo.

Ndiyo mpango mpana zaidi wa amani uliopendekezwa na serikali mjini Kabul, lakini ulikataliwa na Taliban, wanaoitazama serikali ya Ghani kama haramu, na badala yake waliongeza mashambulizi.

Wapiganaji wa Taliban wamefanya shambulizi mjini Wana, Waziristan Kusini, muda baada ya kutangaza mpango wao wa kusitisha mapigano.

Mei 31 wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon ikasema maafisa wa Afghanistan wanajadiliana na Wataliban kuhusu usitishaji mapigano. Siku kadhaa baadae, Juni 7, Ghani akatangaza kilichoonekana kama mpango wa usitishaji mapigano wa upande mmoja na Taliban ili kutoa fursa ya kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr kwa amani, ingawa alisema operesheni dhidi ya makundi mengine likuwemo la Dola la Kiislamu zingeendelea.

Taliban hawakujibu mara moja, na wachambuzi wakaonyesha mashaka, wakati mitandao ya kijamii ikifurika na ujumbe unaowataka Wataliban wakubali. Maafisa wa NATO na Marekani wanasema wanatumai hatua hiyo itapelekea mafanikio.

Kufikia siku ya Jumamosi kundi la Taliban lilitangaza mpango wao wa kihitoria wa kusitisha mapigano kwa muda wa siku tatu za kwanza za Eid. Taarifa yao haikuwa inamjibu moja kwa moja Ghani, lakini tarehe zinagongana.

Hatua hizo zimepokelewa kwa tahadhari na wengi, lakini pia ni ahueni kwa raia na maafisa wa serikali ya Afghanistan waliochohwa na vita. Mchambuzi wa kimagharibi alieko mjini Kabul, aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, kwamba hatua hizo ni za “kujenga imani.”

Lakini suala la iwapo zinapelekea kufikiwa jambi kubwa zaidi bado haliwezi kusemwa kwa uhakika mapaka sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!