Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mpambano mzito Ndugai vs Zitto
Habari za Siasa

Mpambano mzito Ndugai vs Zitto

Spread the love

KESI ya kikatiba inayohusu kinga ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya Bunge kuhoji wenye kinga kuunguruma leo tarehe 15 Februari 2019. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Msingi wa kesi hiyo unatokana na Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri kumtaka Profesa Mussa Asaad kwenda hujielezi mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge kwa madai ya kulidhalilisha Bunge.

Kesi hiyo ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2019 ilifunguliwa na Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu ni dhidi ya Spika Ndugai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Kwenye kesi hiyo Zitto ameiomba mahakama kutoa tafsiri ya kinga ya CAG kwa mujibu wa Katiba ya Nchi.

Pia ameiomba mahakama kutoa tafsiri ya haki, kinga na madaraka ya Bunge katika kushtaki watu wanaodaiwa kudharau Bunge.

Kesi hiyo dhidi ya Spika Ndugai na AG kwa upande wa mashtaka itaongozwa na Wakili Fatuma Karume, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Wakili Karume atakuwa na kazi ya kuhakikisha anaishawishi mahakama kuwa, Bunge halina mamlaka ya kumuhoji Prof. Asaad.

Kwa upande wa Serikali utatakiwa kupangua hoja za Zitto na kuishawishi mahakama kuwa, Prof. Asaad hana kina inayiozungumzwa.

Akiwa nchini Marekani Prof. Asaad alisema kwamba, mhimili huo wa kutunga sheria, umekuwa dhaifu na hivyo umeshindwa kutimiza wajibu wake.

Ndugai alitumia mkutano na wanahabari kuagiza Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, kumhoji Prof. Asaad na baadaye kumshauri yeye hatua za kuchukua.

Akizungumza mjini Dodoma, Ndugai alisema, Prof. Assad, anatakiwa kufika mbele ya kamati hiyo, tarehe 21 Januari 2019, ili kujibu “tuhuma za kudhalilisha Bunge.”

Na kuwa, aliamua kuchukua hatua hiyo, baada ya kujiridhisha kuwa CAG aliliita “Bunge dhaifu.”

Alisema, “…ninamtaka CAG, kufika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, kwa hiari yake, tarehe 21 Januari mwaka huu. Vinginevyo, nitaagiza akamatwe na kuletwa mbele ya kamati kwa pingu.”

Hata hivyo, Prof. Asaad aliutikia wito huyo kwa kudika mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge ambapo mpaka sasa kilichojadiliwa kimebaki kuwa siri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!