Bernard Morrison

Morrison ‘akwea pipa’ kuifuata Kagera

Spread the love

WINGA wa klabu ya Yanga, Bernard Morrison amesafiri kwenda kuungana na kikosi cha Yanga kinachoelekea mkoani Kagera, kuvaana na wenyeji wao Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu siku ya Jumatano, kwenye Uwanja wa Kaitaba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Winga huyo ambaye alisalia Dar es Salaam baada ya kocha wa kikosi hicho, Luc Eymael kusema kuwa hakuwa sehemu ya mpango kwenye mchezo dhidi ya Biashara ambao ulichezwa Mara baada ya kuwa na sintofahamu nyingi licha ya kurejea kwake mazoezini.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, mchezaji huyo aliweka picha ikimuonesha yupo kwenye ndege na kuandika ujumbe mfupi wa maandishi kuwa yupo njiani kuelekea Kagera.

Morrison anakwenda kuongezea nguvu kwenye kikosi hicho baada ya kukosekana kwa muda mrefu na kufanya kuwa sehemu ya maandalizi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba siku ya Jumapili kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho.

Licha ya kwenda kujiunga na wanzake mchezaji huyo hivi karibuni alikuwa kwenye mgogoro na uongozi wa klabu hiyo kwenye masuala ya mkataba, na baadae kutoroka kambini hatua ambayo ilimfanya kocha wa kikosi hiko kumfukuza kwa sababu za utovu wa nidhamu.

Yanga inakwenda kuvaana na Kagera Sugar ambayo waliondosha kwenye michuano ya kombe la shirikisho kwenye hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-1.

WINGA wa klabu ya Yanga, Bernard Morrison amesafiri kwenda kuungana na kikosi cha Yanga kinachoelekea mkoani Kagera, kuvaana na wenyeji wao Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu siku ya Jumatano, kwenye Uwanja wa Kaitaba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam ... (endelea). Winga huyo ambaye alisalia Dar es Salaam baada ya kocha wa kikosi hicho, Luc Eymael kusema kuwa hakuwa sehemu ya mpango kwenye mchezo dhidi ya Biashara ambao ulichezwa Mara baada ya kuwa na sintofahamu nyingi licha ya kurejea kwake mazoezini. Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, mchezaji huyo aliweka picha ikimuonesha yupo kwenye ndege…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!