Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Michezo Morrison aishinda Yanga, kupelekwa kamati ya maadili
Michezo

Morrison aishinda Yanga, kupelekwa kamati ya maadili

Bernard Morrison
Spread the love

BERNARD Morrison amefanikiwa kuibwaga klabu ya Yanga kwenye kesi ya kimakataba iliyokuwa inasikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Kamati hiyo iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Elias Mwanjala ilisikiliza shauli hilo kwa siku tatu mfululizo kabla ya kutoa uamuzi jioni hii leo.

Akisoma uamuzi wa Kamati hiyo Eliasi Mwanjala alisema kuwa mkataba ulioletwa na klabu ya Yanga unaonekana kuwa na mapungufu kiasi cha kukosa uhalali.

“Kuna mapungufu kwenye ukurasa wa kutia sahihi baina ya Morrison na Yanga, umekatwa lakini hakuna sahihi za watu wawili na mkataba lazima wasaini wote ni baadhi ya vitu tumeona vina mapungufu,” alisema Mwanjala.

Baada ya uamuzi huo, Mwanjala aliongezea kuwa mchezaji huyo atapelekwa kwenye kamati ya maadili kutokana na kusaini mkataba na klabu ya Simba huku akiwa na kesi ndani ya shirikisho hilo.

Kesi hiyo ambayo ilivuta hisia za mashabiki wengi wa soka nchini hasa kwa klabu za Simba na Yanga kiasi cha kujazana nje ya ofisi za TFF zilizopo Karume, Ilala jijini Dar es Salaam

Kwa minajili hiyo Morrison atakuwa halali kuchezea klabu ya Simba katika msimu ujao wa mashindao baada ya kuingia nao mkataba wa miaka miwili 8 Agosti, 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

error: Content is protected !!