Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mo Salah aitikisa Liverpool
Habari Mchanganyiko

Mo Salah aitikisa Liverpool

Mohamed Salah
Spread the love

KAULI ya Mohamed Salah, mshambuliaji wa Klabu ya Liverpool kwamba, alifedheheshwa kwa kutopewa nafasi ya unahodha wakati wa mechi yao na Midtjylland, Klabu Bingwa Ulaya imetikisa. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Salah ambaye ana misimu mine tangu kujiunga na klabu hiyo, anahusishwa na kutaka kukimbilia Hispania na kujiunga na Klabu ya Barcelona ama Real Madrid baada ya kuhisi kuonekana ‘kimeo’ kwenye klabu yake ya sasa.

Katika mechi hiyo iliyopigwa tarehe 9 Desemba 2020, Salaa anasema alitarajia kupangwa na hodha lakini kocha wake hakumpa nafasi hiyo.

“Ukweli nilifedheheshwa sasa, nilitarajia kuwa nahodha, lakini ni uamuzi wa meneja hivyo nakubaliana nao,” alisema Salah wakati wa mahojiano na chombo kimoja cha habari cha Hispania.

Kauli hiyo imeibua mkanganyiko mkubwa miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo, huku taarifa za kutaka kuondoka kwake zikizidi kupamba moto.

Jurgrn Klopp, Kocha wa Liverpool alipoulizwa kuhusu kauli ya Salah, alisema hana cha kuongea.

Amesema, ni mara yake ya kwanza kumsikia Salah akilalamikia hilo “…tulicheza Jumapili na Jumatano kwa hivyo tulihitaji kupumzisha miguu. “Klopp alisema na kuongeza “Mo alikosa dakika saba tu katika michezo minne iliyopita.”

Hata hivyo, tayari klabu yake imeeleza kwamba, haina mpango wa kumwachia mshambuliaji huo mwenye mkataba naye mpaka mwaka 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!