Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mmiliki wa Mwendokasi kizimbani kwa uhujumu uchumi
Habari Mchanganyiko

Mmiliki wa Mwendokasi kizimbani kwa uhujumu uchumi

Spread the love

MKURUGENZI wa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (Udart), Robert Kisena na wenzake watatu wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kuhujumu uchumi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Washtakiwa wengine ni pamoja na Kulwa Kisena, Charles Nawe na Chen Shi, Raia wa China.

Leo tarehe 11 Februari 2019 Wakili wa Serikali, George Barasa akisaidiana na Moza Kasubi pamoja na Imani Mitumezizi Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba aliwasomea mashtaka 19 watuhuwa hao.

Shitaka la kwanza ni kula njama ya kufanya uhalifu ambapo watuhumiwa wote  wanadaiwa kati ya tarehe 1 Januari 2011 na tarehe 31 Mei 2018 kwa pamoja na mtu mwingine ambaye hakuwepo mahakamani walidaiwa kula njama ya kufanya uhalifu.

Shitaka la pili ni  kufanya matumizi ya mafuta ya Petroli bila kuthibitisha kinyume na kifungu cha sheria ya Petroli namba 21 ya mwaka 2015 ambapo Robart Kisena  na Kulwa Kisena  wanadaiwa kati ya tarehe 1 Januari 2015 na 31 Desemba 2017 eneo la Jangwani Jiji Dar es Salaam.

Wakiwa kama wakurugenzi wa kampuni ya mafuta ifahamikayo kama Zenon Oil and Gad Limited kwa pamoja walidaiwa kutenda kosa hilo kwa kufanya matengenezo ya miondombinu ya Mafuta ya Petroli kwenye Ofisi za Udart za Jangwani bila kuthibitishwa na Mamlaka ya Nishati na Maji (EWURA).

Shitaka la tatu  ni kufanya mauzo ya mafuta ya Petroli  kinyume cha Sheria ambapo Robert Kisena  na Kulwa Kisena  wanadaiwa kati ya tarehe 1 Januari 2015 na 31 Desemba 2017 eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam wakiwa kama wakurugenzi wa kampuni ya mafuta ya Zenon Oil and Gad Limited kwa pamoja walifanya mauzo ya mafuta ya petroli kwenye mabasi ya mwendokasi kinyume cha sheria.

Shitaka la nne ni wizi ambao mshitakiwa wa kwanza na wapili wakiwa kama wakurugenzi wa mabasi yaendayo kasi  (UDART) na mshitakiwa wa tatu kwa pamoja kati ya tarehe 25 Mei 2015 na 31 Desemba 2016 jijini Dar es Salam wanadaiwa kuiba Sh. 1.2 bilioni mali ya Udart.

Shitaka la tano na la sita matuhumiwa namba moja, mbili na tatu wanatuhumiwa kufanya utakatishaji fedha. Ambapo inadaiwa kati ya terehe 25 Mei 2015 na 31 Desemba 2016  watuhumiwa hao walitakatisha kiasi cha Sh. 1.2 bilioni ambazo walijua kuwa ni zao la fedha haramu.

Shitaka la saba ni kulaghai ambapo inadaiwa kuwa mshtakiwa namba moja Robart Kisena na mshitakiwa namba nne Chen Shi siku ya tarehe 20 Oktoba mwaka 2012  jijini Dar es Salama walitengeneza nyaraka ya uongo yenye jina la Extract Board Resolution.

Nyaraka hizo zilionesha kuwa watendaji wa Longway Engineering Company Limeted imefungua akaunti kwenye benki ya KCB tawi la Tanzania kitu ambacho si kweli.

Shitaka la nane  kutumia nyakara za uongo ambapo mshtakiwa namba moja Robart Kisena na mshatakiwa namba nne Chen Shi siku ya tarehe 20 Oktoba 2012  jijini Dar es Salama walitengeneza nyaraka ya uongo yenye jina la Extract Board Resolution  iliyokuwa ikionesha kuwa watendaji wa Longway Engineering Company Limeted imefungua akaunti kwenye benki ya KCB tawi la Tanzania kitu si kweli.

Shitaka la tisa hadi 10 linamkabili mshtakiwa namba moja Robart Kisena na mshatakiwa namba nne Chen Shi ambao wanaidaiwa siku ya tarehe 20 Oktoba mwaka 2012 walifanya ulaghai kwa kutengeneza nyaraka ya uongo yenye kutaka orodha ya  wamiliki wa shea kwenye kampuni ya Longway Engineering Company kwa na kufungua akaunti kwenye benki ya KCB tawi la Tanzania.

Shitaka la 11 linamkabili mshitakiwa Robart Kisena ambaye anadaiwa kuwa siku ya tarehe 6 Aprili mwaka 2016 akiwa kwenye Benki ya KCB tawi la Ilala jijini Dar es Salaam alitengeneza nyaraka ya uongo ya kuhamisha fedha ambapo alihamisha zaidi ya Sh. 594 milioni kama malipo ya wafanyakazi wa kampuni ya  Longway Engineering.

Shitaka la 12 na 13 linamkabili mshtakiwa namba moja ambapo anadaiwa kughushi nyaraka na kuijiingizia pesa kwa njia ya kulaghai ambapo inadaiwa kati ya tarehe 6 Aprili alijiingizia Sh 594 milioni na 8 Juni mwaka 2016 mtuhumiwa alijiingizia 594 milioni kwa kughushi nyaraka

Shitaka la 14 na 18 ni utakatishaji fedha ambapo mtuhumiwa namba moja na nne  wanadaiwa tarehe 8 Aprili mwaka 2016 kwenye Benki ya NMB tawi la Ilala watuhumiwa  wametakatisha fedha kiasi cha Sh. 594 na tarehe 26 Mei, 2016  walitakatisha kiasi cha zaidi Sh 600 milioni.

Shtaka la 15, 16 na 17 ni kughushi, kutengeneza nyaraka za uongo na kuingizia fedha kwa njia za ulaghai ambapo mshitakiwa Robart Kisena na Chen Shi .

Kosa la 15 lilifanya siku ya tarehe 26 Mei mwaka 2016 eneo la Ilala kwenye Benki ya NMB tawi la Ilala na Kosa la 16 lifanywa tarehe 30 Mei Mwaka 2016 eneo hilo hilo ambapo wanadaiwa kughushi na kutengeneza nyaraka za uongo ili kujiingizia Sh 75 Milioni.

Na kwenye shitaka la 17 watuhumiwa  walijiingizia zaidi ya Sh. 600 milioni kwa kwa uongo. Washatakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama kuwasihi upande wa Mashtaka kuwahisha upepelelezi ili kesi hiyo isikilizwe.

Kesi hiyo imehailishwa hadi tarehe 23 Februari, mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!