Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mkurugenzi Dodoma ajitosa migogoro ya ardhi
Habari za Siasa

Mkurugenzi Dodoma ajitosa migogoro ya ardhi

Spread the love

MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema  migogoro yote ambayo inatokana na kero za ardhi ndani ya jiji ni lazima itatuliwe kwa mujibu wa seria ya ardhi na kila mtu apate haki yake. Anaripoti Danny Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na kutaka migogoro ya ardhi kuatuliwa amevunja kamati ya upimaji ya ardhi katika kata ya Mnadani kwa maelezo kuwa kamati hiyo imekuwa ikisababisha kuwepo kwa migogoro ardhi na kero lukuki  kutokana na kamati hiyo kutofanya kazi kwa uadilifu.

Kutokana na hali hiyo Kunambi ametoa onyo na kueleza kuwa mtu atakayebainika kufanya vurugu kwa lengo la kukwamisha mpango mpya wa urasimishaji ardhi katika mitaa ya Kata  ya Mnadani atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kunambi ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa mtaa wa Ndachi na maeneo jirani kuhusiana na mpango mpya wa urasimishaji ardhi kwa lengo la kupunguza ama kumaliza migogoro ya ardhi.

Alisema baada ya maagizo ya Mkuu wa Mkoa, Dk. Binilith Mahenge aliyoyatoa siku za nyuma la kutaka kuaza kwa mchakato wa kurasimisha ardhi katika maeneo ambayo hayakupiwa na yalikuwa na migogoro ya ardhi.

” Wote mnakumbuka tulikuja hapa na mkuu wa mkoa (Dk. Binilith Mahenge) na aliagiza kuanza kwa mchakato wa kurasimisha ardhi na kamati ziliundwa, lakini mchakato huu umeonekana kukwama katika mitaa mitatu ya Mbwanga, Mnadani na Ndanchi.

“Na hii inatokana na watu wachache ambao wanataka kutumia mpango huu kujinufaisha binafsi na kuibua mivutano isiyo na sababu. Tuache siasa au kujipatia umaarufu kupitia changamoto za wananchi. Sasa baada ya mpango mpya kuanza, mtu yeyote atakayevuruga au kukwamisha basi mahakamani kutakuwa nyumbani kwake,” alisema.

Kunambi ambaye aliwataka wananchi kuhakikisha hawazirudishi kampuni mbili za urasimishaji ardhi zilizoingia kwenye mgororo, sambamba na moja aliyoidai kushindwa kazi katika maeneo mengi, alitoa orodha ya kampuni ambazo zimesajiliwa na serikali.

“Natoa orodha hii itakaa ofisi ya mtendaji mwananchi unahaki ya kutoa nakala, ila hakikisheni zile zilizochangia kukwamisha mchakato wa awali hazipewi kazi, Serikali inataka maeneo yenu yarasimishwe ili tulete miundombinu ya maji, umeme na huduma zingine za kijamii,” alisema.

Aidha, Kunambi alitumia nafasi hiyo kuwagiza watendaji wa serikali kuhakikisha wanaitisha mikutano ya wananchi isikapo Jumanne ili wachague kamati mpya ya watu saba kwa kila mtaa ambao ndio watakaosimamia suala hilo, huku akiwataka wananchi kuwa makini katika kuchangua wajumbe.

“Msifanye kosa kwenye kuchagua wajumbe wa kamati, mkiwachangua wala rushwa au madalali wa viwanja wanaweza kukwama tena kama awali, kwani kuna baadhi yalitaka kujipiatia viwanja kupitia ardhi zenu,” alisema.

Aidha, Kunambi alisema baadha ya kufanyika urasimishaji huo, wananchi ambao maeneo yao yatapisha miundombinu ya huduma za kijamii watapewa maeneo mbadala na kusisitiza kuwa hakuna mtu yeyote atakayepoteza haki yaki.

Kuhusu fedha walizotoa kwenye mchakato wa awami, Kunambi alisema fedhahizo ziko salama na kuwa zitatumika kwenye mpango mpya na kuonya mtu yeyote asithubitu kuhukua hata senti moja ya fedha hizo. Pia alisisitiza kuwa mwongozi wa gharama za kazi hiyo ni kati ya Sh. 200,000-hadi Sh 250,000.

” Kuna kampuni ilisema ingefanya kazi hiyo kwa Sh. 150,000, watu kama hawa wanatoa bei ndogo ili mvutia, lakini mujue watafidia fedha zao kupitia ardhi yenu wenyewe. Hivyo mnatakiwa kuwa kati ya kiwango kilichowekwa,” alisema.

Naye mwananchi Paul Mashinene alisema mgogoro uliibuka baada ya kutokea kampuni moja ambayo ikitaka kufanya urasimishaji kwa Sh. 250,000 na nyingine Sh. 150,000 jambo ambalo liliwafanya wananchi kuwa na mashaka kuwa huwenda wanaibiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!