Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkoa wa Mwanza waahidi neema kwa wafanyabishara
Habari Mchanganyiko

Mkoa wa Mwanza waahidi neema kwa wafanyabishara

Taswila ya jiji la Mwanza
Spread the love

SERIKALI imeahidi kushirikiana na wafanyabiashara nchini ili kukuza biashara zao na uchumi wa taifa kwa kuhakikisha bidhaa zao zinapata soko la uhakika kimataifa, anaandika Moses Mseti.

Imesema itawasaidia wafanyabiashara hao ili kuwaondolea vikwazo katika soko la nje na imekusudia kwamba kilimo kinakuwa ni kichocheo kikubwa kwenye ukuaji wa uchumi nchini.

Kauli hiyo imetolewa na John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika uzinduzi wa maonyesho ya 12 ya kibiashara ya Afrika Mashariki yaliyofanyika jijini hapa.

Mongella amesema serikali imejipanga kuhakikisha inawasaidia wafanyabiashara wa ndani kwenye soko la nje kushindanisha bidhaa zao nje ya nchi ili za ndani ziweze kupata soko la uhakika.

“Kama kuna mfanyabiashara anapata kikwazo katika biashara zake, afike ofisini kwangu kuangalia ni namna gani tunaweza kumpa msaada katika eneo lolote lile ambalo ameshindwa kupata msaada kwenye ofisi za umma.

“Wafanyabiashara nchini changamkieni fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo katika soko la pamoja la Afrika Mashariki ikiwemo fursa ya kuuziana bidhaa wenyewe kwa wenyewe na kuleta tija kwa watu wetu badala ya kutegemea masoko ya nje ambayo pia yamekuwa hayana uhakika sana,” amesema Mongella.

Amesema maonyesho hayo yanaweza kuimarisha mahusiano ya kibiashara kwa kubadilishana, ujuzi, uzoefu, ubunifu, mazingira ya biashara katika eneo husika na kujifunza mbinu mbalimbali katika kukuza uuzaji wa bidhaa nje kutumia fursa zilizopo masoko ya Afrika Mashariki, SADC, AGOA.

Joseph Kahungwa, Makamu wa Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania ( TCCIA), amesema viwanda ni chachu katika kukuza shughuli za uchumi nchini huku akiiomba serikali iendelee kuboresha mazingira ikiwemo sera na sheria zinazosimamia shughuli za kiuchumi.

Elibariki Mmari, Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabuashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) mkoa wa Mwanza, amesema maonyesho hayo yaliyoanza na washiriki 48, kwa sasa washiriki wa maonyesho hayo imeongezeka na kufikia zaidi ya 220 Kutoka nchi za Kenya, Uganda, India, China, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.

Amesema bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa uwanja maalum wa kufanyia maonyesho hayo hivyo aliomba serikali ya mkoa kuwapatia eneo ambalo watajenga uwanja wa kisasa wa maonyesho ya Afrika Mashariki yatakayoendana na mazingira ya kisasa ya kiuchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

error: Content is protected !!