Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mkataba wa Muungano watikisa Bunge
Habari za Siasa

Mkataba wa Muungano watikisa Bunge

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

MNYUKANO mkali umeibuka bungeni, baada ya baadhi ya wabunge kuhoji kuwapo kwa vifungu vya Katiba ya Zanzibar, vinavyopingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akichangia bajeti ya ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano), bungeni jana mjini Dodoma, mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amesema, kukinzana kwa Katiba ya Muungano na ile ya Zanzibar, kunahatarisha uhai wa Muungano wenyewe.

Alitoa mfano wa vifungu kadhaa alivyodai kuwa vimekuwapo na mgongano mkubwa na Katiba ya Muungano yam waka 1977.

Alisema, “mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya Kwanza ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 inasema, ‘Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake, ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

“Katika Ibara yake ya 2 inatamka, ‘Zanzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Masharti haya, ni kinyume na Katiba ya Muungano Ibara ya 1 inayotamka Tanzania ni Nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.’”

 Akiendelea kuchambua utata huo wa Katiba, Kubenea alisema, “katika Ibara ya 26, Katiba ya Zanzibar inatamka kwamba Rais wa Zanzibar ni Mkuu wa Nchi ya Zanzibar.

 “Lakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 33(2) inasema, Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.”

 Aidha, Kubenea amesema, Ibara ya 2A ya Katiba ya Zanzibar inatamka kwamba kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

 “Mheshimiwa Naibu Spika, “masharti haya ni kinyume na Ibara ya 2 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano,” ameeleza Kubenea.

Ameongeza: “Ibara ya 2(2) imetamka kuwa kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge:

“Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo.”

 Akizungumzia Ibara ya 132 ya Katiba ya Zanzibar, Kubenea alisema, Katiba hiyo inaeleza kuwa hakuna Sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka Sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. 

Alisema, Katiba inataka sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika. 

Alisema, ibara hii inaeleza zaidi, pale Sheria ndogo inapoundwa kwa mujibu wa uwezo uliowekwa chini ya kijifungu cha 132(1) na (2) itatumika tu pale itakapotimiza shuruti zote zilizowekwa kwa matumizi ya Sheria Mama kama ilivyoainishwa katika kifungu hicho.

 “Masharti haya, ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ambapo Ibara ya 64 inatamka kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano ndilo lenye mamlaka ya kutunga sheria kwa mambo ya Muungano (Bara na Zanzibar) na yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara,” amefafanua.

Alitaja kifungu chenye utata kuwa ni Sura ya 3 juu ya Kinga ya Haki za Lazima, Wajibu na Uhuru wa Mtu Binafsi.

Kwamba, Ibara ya 24(3) inatamka kwamba, Rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu (Zanzibar), katika shauri lililofunguliwa dhidi ya masharti ya Sura hii ya Katiba yatasikilizwa na Mahakama Kuu (Zanzibar) mbele ya Majaji watatu bila ya kumjumuisha Jaji aliyeamua shauri hilo mara ya kwanza. 

Anasema, Katiba inaeleza kuwa majaji hao watatu watateuliwa na Jaji Mkuu na uamuzi wao utakuwa ni wa mwisho na hautokatiwa rufaa kwenye Mahkama ya Rufaa ya Tanzania.

 “Lakini ni wazi kwamba masharti haya ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 117(1) na (4) ambayo inatamka kwamba Mahakama ya Rufani ndiyo yenye Mamlaka ya juu ya kutoa haki nchini na uamuzi wake ni wa mwisho.”

 Wabunge waliochangia hoja hiyo, ni pamoja na Ally Salehe ambaye alidai kuwa baadhi ya kero za Muungano, zimesababisha wananchi kuuchukia Muungano wenyewe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!