Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mkapa 1938 – 2020: Kikwete ‘jana tu nilizungumza naye’
Habari za Siasa

Mkapa 1938 – 2020: Kikwete ‘jana tu nilizungumza naye’

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha maombelezo nyumbani kwa Marehemu Benjamin Mkapa
Spread the love

RAIS Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete amesema, jana tarehe 23 Julai 2020 alikwenda kumtembelea Mzee Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu hospitali kabla ya kufa kwake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

“Unajua kifo ni siri ya Mungu. Jana jioni tu nilikwenda kumuona hospitali na tulizungumza sana, alikuwa sio mtu unayeweza kusema anaumwa sana.

“Alikuwa na maumivu ya kawaida tu. Hakuwa mgonjwa wa kumtilia mashaka. Tumkumbuke kwa yale aliyosimamia na kupigania katika maisha yake,” amesema Rais Kikwete.

Dk. Kikwete ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kufika nyumbani kwa Mkapa, Msasaji jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa waliofika nyumbani hapo ni Sheikh Aboubakar Zuberi, Mufti Mkuu wa Tanzania. Amewataka Watanzania kuwa na subira katika kipindi hiki  cha kuondokewa na kiongozi aliyeliongoza taifa hili.

“Neno langi ni kuwa na subira katika msiba huu mzito kwenye kipindi hiki,” amesema Mufti Zuberi.

Kwa wakati tofauti kupitia kurasa zao za twitter, viongozi wa zamani, wanasiasa, wanaharakati na wananchi wameonesha kuguswa na msiba huo mzito uliolikumba Taifa.

Frederick Sumaye, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, amesema atamkumbuka Rais Mkapa kutokana na utendaji kazi wake na uzalendo kwa Taifa.

Sumaye amesema Rais Mkapa alikuwa si mtu wa kuingilia majukumu ya wasaidizi wake, na kwamba katika uongozi wake watumishi wake walikuwa na uhuru wa kufanya kazi.

“Mzee Mkapa hata baada ya kustaafu nchi nyingi zilimtumia mahali ambapo kuna jambo linahitaji utatuzi, alijenga heshima, ni kiongozi ambaye alikuwa hakuingilii kwenye kazi kulikuwa na uhuru wa kufanya kazi na kusimamia mambo ya Serikali bila uwoga,” amesema Sumaye.

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, amesema Watanzania wampata majonzi kufuatia msiba wa Rais Mkapka.

 “Ni majonzi makubwa kwa Tanzania! Tumuombee Mzee wetu Mhe Rais Mstaafu Benjamin Mkapa apumzike kwa Amani. Natoa pole kwa mke wa marehemu Mama Anna Mkapa, watoto, familia, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wote. Bwana ametoa, bwana ametwaa,” ameandika Waziri Ummy

Mzee Pius Msekwa, Spika Mstaafu wa Bunge amesema, Taifa limepoteza kiongozi mahiri.

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema, msiba wa Rais Mkapa ni pigo kwa taifa.

‘Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Rais Mkapa, Rais wa Tanzania mwaka 1995 hadi 2005, ni pigo kwa Watanzania, salamu zangu za pole ziende kwa ndugu na Watanzania wote,” ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter.

Mfanyabiashara Mohammed Dewji, amesema msiba wa Rais Mkapa ni mzito, na kutoa pole kwa walioguswa na msiba huo mzito.

“Bado ni ngumu kukubali kwamba Mzee Mkapa hatunaye tena. Pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania kwa ujumla kwa msiba huu mzito. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi,” ameandika Mo Dewji.

January Makamba, Mbunge wa Bumbuli anayemaliza muda wake naye katika ukurasa wake wa Twitter ameomboleza msiba huo kwa kuandika “ Bado ni vigumu kukubali kwamba Mzee Mkapa hatunaye tena. Nimsiba mzito kwa Taifa letu, Mungu amlaze pema peponi.”

Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo amesema amepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa, na kutoa pole kwa walioguswa na msiba huo.

“Nimepokea kwa mshtuko taarifa za msiba wa Mzee wetu Mkapa, kama ambavyo Rais John Magufuli alivisema wakati akitutangaza Watanzania,” ameandika Bashe katika ukurasa wake wa Twitter.

Richard Kasesea, Mkuu wa Wilaya ya Iringa amesema atakumbuka maneno ya Rais Mkapa.

“RIP baba yetu Mzee Mkapa, bado nakumbuka maneno yako mzee wetu,” ameandika Kasesela.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) kimetuma salamu za rambi rambi kufuatia kifo hicho,

Kupitia ukurasa wake wa Twitter LHRC imeomboleza msiba huo kwa kuandika “LHRC tunatuma salamu za rambirambi kwa Rais John Magufuli, familia ya Mheshimiwa Mkapa na atanznia wote kwa msiba huu mkubwa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!