Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkakati wa serikali kwa bodaboda ni huu
Habari Mchanganyiko

Mkakati wa serikali kwa bodaboda ni huu

Anthony Mavunde, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira.
Spread the love

SERIKALI imeainisha mikakati mitano inayofanya katika kuwajengea uwezo waendesha bodaboda ukiwemo faida za kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Antony Mavunde, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Kazi na Ajira wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Lushoto, Shabani Shekilindi (CCM).

Katika swali hilo, mbunge huyo alisema uendeshaji bodaboda ni ajira kama zilivyo ajira nyingine nchini.

Amehoji, Serikali ina mpango gani wa kuwajengea uwezo vijana hao ili kuifanya kazi yao hiyo iwe rasmi na yenye kutambulika kama kazi nyingine zozote.

Akifafanua Mavunde amesema, mipango hiyo ni pamoja na kutoa mafunzo ya udereva kupitia Jeshi la Polisi kwa waendesha bodaboda na hatimaye kupatiwa leseni za udereva.

Aidha, kama ilivyo vyombo vingine vinavyotoa huduma za usafiridhaji, usalama wa waendesha bodaboda na abiria umeendelea kusimamiwa na kulindwa wanapotekeleza majukumu yao barabarani.

Mwingine ni kuhamasisha uundwaji wa vikundi vya waendesha bodaboda ili hatimaye viweze kuwezeshwa kwa mitaji na mafunzo kupitia mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na wadaiu wengine.

Aidha, kuwapatia maeneo ya kuegesha bodaboda ya kuyatambua pamoja na kuwapatia vitambulisho.

Pia, kuwapatia waendesha bodaboda mafunzo ya ujasiriamali na hatimaye kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu na kuwaunganisha na taasisi zingine zinazotoa mikopo.

Na kuwa, watapatiwa elimu juu ya faida za kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na kuwaunganisha na mifuko husika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!