Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Milioni 4.9 zamkamatisha kigogo wa Takukuru
Habari Mchanganyiko

Milioni 4.9 zamkamatisha kigogo wa Takukuru

Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani
Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania, imemkamata ofisa wake wa uchunguzi mwandamizi, Nina Sipilon Saibul kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh.4.9 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kinondoni … (endelea).

Taarifa iliyotolewa jana Ijumaa tarehe 11 Septemba 2020 na Doreen Kapwani, Ofisa Uhusiano wa Takukuru imesema, Nina alikamatwa jana Alhamisi.

Doreen alisema, Nina ambaye ni Afisa Uchunguzi ofisi ya Takukuru Kinondoni jijini Dar es Salaam, aliomba rushwa kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wa Jiji hilo anayejishughulisha na shughuli za Real Estate.

“Takukuru Mkoa wa Kinondoni, ilipokea taarifa za malalamiko dhidi ya afisa wake, kuomba rushwa ili asiendelee na uchunguzi uliodaiwa ulikuwa ukiendelea ndani ya Takukuru dhidi ya mfanyabiashara huyo(mlalamikaji).”

“Baada ya taarifa hizo kupokelewa, uchunguzi wa awali wa kuthibitisha tuhuma hizo ulifanyika na kubaini upo ukweli wa madai ya kuomba hongo lakini hakukuwa na jalada wala uchunguzi wowote uliokuwa ukiendelea dhidi ya mlalamikaji,” amesema Doreen.

Alisema, Takukuru imechukua hatua hii ili kuhakikisha inajisafisha dhidi ya watumishi wake wachache wenye tabia ovu zenye kukichafua chombo hicho.

“Uchunguzi dhidi ya tuhuma hii unakamilishwa ili kuweza kuwafikisha watuhumiwa mahakamani mapema iwezekanavyo,” alisema Doreen.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!