Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Milioni 32 zanunua gari la wagonjwa Bukoli-Geita
Habari Mchanganyiko

Milioni 32 zanunua gari la wagonjwa Bukoli-Geita

Spread the love

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Rafiki Surgical Mission kutoka nchini Australia wametoa msaada wa gari la wagonjwa lenye gharama ya Sh.32 milioni kuhudumia wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Bukoli na maeneo jirani wilayani Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya gari hilo jana Jumanne tarehe 29 Septemba 2020 katika Kituo cha Bukoli mkoani Geita, Makamu Rais anayeshughulikia Mahusiano na Maendeleo endelevu, Simon Shayo alisema, msaada wa gari hilo umetolewa kwa wakati kwani utasaidia kutatua changamoto za usafiri kwa wagonjwa mahututi kwenye kata hiyo ya Bukoli na maeneo ya jirani.

“Halmashauri ya Wilaya ya Geita iliomba msaada wa gari la wagonjwa kutoka GGML ili kuwasaidia wagonjwa katika jamii ya watu wa Bukoli ambao waliokuwa na changamoto kubwa kila ilipobidi kusafirisha wagonjwa kwa ajili matibabu makubwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Geita ambayo ipo wastani wa kilomita 35 kutoka kijiji cha Bukoli,” alisema

“Ushirikiano kati yetu na Rafiki Surgical Mission ni mwitiko wa maombi hayo na umekuja muda mwafaka kwa kuwa wamekuwa pia na dhamira ya kusaidia huduma za afya mkoani Geita kwa miaka kadhaa sasa,” alisema Shayo.

Shayo alisema, karibu miaka 20 sasa, mbali na kutoa msaada wa vifaa tiba, Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na Rafiki Surgical Mission wameongeza wigo wa matibabu kwa watoto na watu wazima mkoani Geita ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya midomo sungura na migongo wazi kwa kuwapatia matibabu ya upasuaji bure.

Alisema GGML pia walitoa msaada katika kituo cha afya cha Bukoli mwaka 2004 kwa kujenga jengo la Wagonjwa wa Nje (Outpatient Department) na nyumba ya watoa huduma wa afya.

GGML imefadhili miradi mbalimbali ya afya wilayani Geita ikiwemo ukarabati wa Hospitali ya Rufaa mkoani Geita na ujenzi wa vituo vipya vya afya katika vijiji vya Nyamalembo, Nyakahongola, Kasota na Kakubiro ambapo miradi yote hiyo kwa pamoja iligharimu Sh.18 bilioni.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ali Kidwaka kwa niaba ya Serikali ametambua mchango wa GGML katika kutatua changamoto ya huduma za afya kwenye halmashauri ya wilaya na kwengineko mkoani Geita na kuwaomba washirika wengine waliopo katika Wilaya ya Geita kushirikiana na Serikali kwa lengo hilo hilo.

Aidha mwaka 2019, GGML ilichangia pia vifaa tiba vyenye gharama ya Sh.142 milioni katika vituo vya afya vya Katoro na Bukoli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!