May 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Milioni 16 wapona corona duniani

Spread the love

WAGONJWA milioni 16.08 wamepoma virusi vya corona (COVID-19) duniani. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mtandao wa worldometer umeripoti leo Jumatatu tarehe 24 Agosti 2020, kuwa maambukizo ya corona dunia yamefikia milioni 23.58 na waliofariki kutokana na ugonjwa huo ni 812,537.

Marekani imeendelea kuwa Taifa linaloongoza kwa maambukizo milioni 5.8, waliopona wakiwa milioni milioni 3.1 na waliofariki dunia wakiwa 180,604.

Brazil inafuatia ikiwa na wagonjwa milioni 3.6, waliopona milioni 2.7 na waliopoteza maisha wakiwa 114,772.

China ambako virusi hivyo vilianzia, iko nafasi ya 35 ikiwa na wagonjwa 84,967, waliopona 79,925 na waliopoteza maisha ni 4,634.

error: Content is protected !!