Tuesday , 16 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Migogoro ya wafugaji kutafutiwa dawa
Habari Mchanganyiko

Migogoro ya wafugaji kutafutiwa dawa

Wafigaji
Spread the love

SERIKALI imewataka viongozi wa Chama cha Wafugaji nchini pamoja na watetezi wa haki za wafugaji kuhakikisha wanaondoa migogoro ya wafugaji na wakulima ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara nchini na hivyo kurudisha maendeleo nyuma, anaandika Mwandishi wetu.

Akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya siku tatu iliyowakutanisha watetezi wa haki za wafugaji nchini, Katibu Tawala  Wialaya ya Arusha, David Mwakiposa, alisema, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo hao watetezi ili waweze kuondoa migogoro inayojitokeza katika jamii.

“Serikali tunaomba sana watetezi wa haki za wafugaji kuangalia kwa uzito wa kipekee kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima na wahamasishe uwanzishwaji wa viwanda vya kuchakata bidhaa za mifugo ili kumuunga mkono Rais Magufuli katika sera ya viwanda,” alisema Mwakiposa

Aidha alisema sekta ya wafugaji na kilimo inaajiri Watanzania walio wengi zaidia asilimia 70 na ndio sekta pekee ambayo haiitaji elimu kubwa tofauti na ajira za viwandani na sehemu nyingine hivyo ni muhimu kujengwa uwezo ili kutimiza sera ya viwanda hapa nchini

Kwa  upande wake Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, (THRDC),  Onesmo Ole Ngurumo alisema kuwa ni vizuri wakajengewa uwezo katika sera ,sheria na mifumo ya utoaji haki katika taifa hili na nje ya nchi ili waweze kutetea vizuri wafugaji

“Tunaamini kuwa watetezi hawa wakifahamu vizu sera na sheria wataweza kuangalia mifumo ya utoaji haki kama haitendeki  kwa wafugaji wataweza kutumia fursa hiyo kuwatetea vizuri,” alisema

Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania, Maghembe Makoye, alisema Tanzania ina mifugo na wafugaji wengi hivyo ni muhimu sana sekta hiyo kujengewa uelewa na kujielekeza kuunda mabaraza ya usuluishi katika ngazi ya vijiji,kata,tarafa hadi wilaya ili kuhakikisha kundi hilo haligombani.

“Ni vizuri tukihamasishana kufuga kisasa ili kujiongezea tija katika uzalishaji wa bidhaa za wafugaji sanjari na kupata masoko ndani na nje ya nchi,“alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Sekta binafsi yasifu utekelezaji wa Mkumbi

Spread the loveSERIKAL imepongezwa kwa utekelezaji wa mapendekezo ya sekta binafsi kupitia...

Habari Mchanganyiko

Kamati ya bunge yapigia chapuo kilimo ikolojia

Spread the loveSERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeshauriwa kushirikiana na wadau wa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yapata hasara 113 milioni hospitali kuwapa misamaha wagonjwa wasiostahili

Spread the loveSERIKALI imepata hasara ya kiasi cha Sh. 111.76 milioni, baada...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!