Mgombea Urais Chadema Z’bar: Nina wake watatu, watoto kumi ninaweza

Spread the love

SAID Issa Mohamed, ameteuliwa na Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwa mgombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 27 na 28 Oktob, 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Mkutano huo umemteua leo Jumanne tarehe 4 Agosti 2020 kuwa mgombea urais kwa kura za wazi.

Baada ya kupigwa kwa kura hizo, Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema amesema “ninamtangaza rasmi Said Issa Mohamed kuwa mgombea wetu wa urais wa Zanzibar.”

Kabla ya kuteuliwa, Mohamed ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Chadema-Zanzibar alipewa fursa ya kuwaomba wajumbe wampe ridhaa kwenda kupeperusha bendera ya Zanzibar.

Amesema ameshika nafasi ya makamu mwenyekiti akiwa na miaka 29, “nimeitumikia kwa ujasiri, unyenyekevu mkubwa na hata mara moja sijawahi kuwa msaliti, mchochezi ndani ya chama hiki.”

“Nimeshiriki kujenga na kusimika chama hiki ndani ya kanda zote, hakuna wilaya au mkoa ndani ya Tanzania bara na Zanzibar zijafika kujenga chama. Nimesimika chama Lindi na Mtwara na leo huko ni wera wera,” amesema

Mohamed amesema “nimesimama mbele yenu ili kupata ridhaa ya kwenda kugombea Zanzibar. Kuna watu wanauliza chini chini nimeona, nimeona wake watatu,” amesema huku shangwe zikiendelea.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema

“Kwetu tulizaliwa 13 na 12 tupo hai. Mimi mwenyewe nina watoto kumi. Ninapokuja kuomba kugombea ninaweza sekta zote. Kuwa na watoto kumi na wake watatu naweza na ninatosha,” amesema Mohamed

SAID Issa Mohamed, ameteuliwa na Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwa mgombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 27 na 28 Oktob, 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea) Mkutano huo umemteua leo Jumanne tarehe 4 Agosti 2020 kuwa mgombea urais kwa kura za wazi. Baada ya kupigwa kwa kura hizo, Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema amesema “ninamtangaza rasmi Said Issa Mohamed kuwa mgombea wetu wa urais wa Zanzibar.” Kabla ya kuteuliwa, Mohamed ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Chadema-Zanzibar alipewa fursa ya kuwaomba wajumbe wampe ridhaa kwenda kupeperusha bendera ya Zanzibar.…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!