Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mgombea udiwani CUF aangua kilio kwenye kampeni
Habari za Siasa

Mgombea udiwani CUF aangua kilio kwenye kampeni

Salum Mwinyikheri, (Katikati) mgombea udiwani katika Kata ya Mumbaka, Masasi mkoani Mtwara akibembelewa na wenzake
Spread the love

SALUM Mwinyikheri, mgombea udiwani katika Kata ya Mumbaka, Masasi mkoani Mtwara, ameangua kilio mbele ya wananchi wakati akiomba kura. Anaripoti Mwandishi Wetu, Masasi … (endelea).

Akihutubia wananchi wake kwenye mkutano aliouandaa, Mwinyikheri alianza kumwaga machozi na kufuatiwa na kilio cha kwikwi akieleza kuumizwa na changamoto zilizopo kwenye kata hiyo, hasa mgogoro wa ardhi na umilikiswaji ardhi.

Kabla ya kuanza kububujikwa machozi, Mwinyikheri alisema kata hiyo ina matatizo mengi na kama angepata ridhaa ya wananchi, angetumia uwezo wake wote kumaliza changamoto hizo na kufanya kata hiyo iwe mahali salama pa kuishi.

Wakati akizungumza maneno hayo, ghafla mgombea huyo alianza kufuta machozi huku yakiongezeka kutiririka. Baadaye baadhi ya viongozi wenzake walimfuata na kumbembeleza huku akitoa kwikwi za kilio.

“Kinachonitoa machozi hapa ni kuwa, natamani sana kuwa diwani wa hapa ili niwasaidie wananchi wa kata hii maana wana changamoto nyingi ikiwemo maji, barabara, afya kwa kinamama wajawazito na migogoro ya ardhi,” amesema.

Prof. Ibrahim Lipumba

Alisema, wananchi wa kata hiyo hawapaswi kufanya makosa kwa kuwachagua wagombea kutoka nje ya CUF, na kwamba wagombea wa chama chake watakapochaguliwa, wataona mabadiliko kwa muda mfupi.

“Ili tupate maendeleo ya haraka, wananchi wanapaswa kuchagua wagombea wa CUF kuanzia udiwani, ubunge na urais,” alisema Mwinyikheri.

Mgombea huo hakuweza kumaliza hotuba yake baada ya kuangua kilio, viongozi na baadhi ya wanachama walimfuata na kuanza kumbembeleza na kisha kumtoa uwanjani na kumpeleka kuketi kwenye kiti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!